Meridian Bet Tanzania

Meridian Bet Tanzania ni waendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini Tanzania. Kampuni hiyo ina leseni ya kuendesha michezo ya bahati nasibu katika sekta zote za ubashiri, ikiwa ni pamoja na maduka ya kubashiri[1] na ubashiri wa mtandaoni[2]. Mpaka sasa, Meridian Bet inaendesha shughuli zake katika mikoa yote Tanzania.[3]

Meridian Bet Tanzania
Limeanzishwa2017
Parent organisation
Bit Tech Limited

Historia

hariri

Meridian Bet Tanzania ilianzishwa mwezi Juni mwaka 2017. Taasisi hii inamilikiwa na kampuni ya Bit Tech Limited, kampuni yenye leseni ya kufanya kazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usajili wa namba 135726 kutoka kwa Mamlaka ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania. Kwa sasa kampuni ya Meridian Bet Tanzania inaendesha biashara zake katika miji takribani yote nchini Tanzania.

Mfumo wa biashara

hariri

Biashara kubwa ya Meridianbet Tanzania ni ya kuendesha biashara ya Kubashiri Michezo, lakini pia Kasino ya Mtandaoni na Sloti. Imepewa leseni kwa ajili ya Kubashiri kwa Njia ya Ujumbe Mfupi USSD Ilihifadhiwa 11 Septemba 2021 kwenye Wayback Machine. kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).[4]

Washirika

hariri

Meridian Bet Tanzania ina washirika wengi wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Meridian Gaming ambao hufanya usambazaji wa programu za kubashiri michezo na kasino za mtandaoni kwenye maduka yake na vilevile kwenye mitandao.[5]

Bidhaa na Huduma

hariri

Meridian Bet Tanzania inafanya kazi katika maduka 100 ya kubetisha na vile vile katika tovuti yake ya mtandaoni. Lengo kuu la kampuni hii ni kujikita katika Kubashiri Michezo (kabla ya mechi kuanza na pale zinapokuwa zimeanza) na vile vile kutoa huduma zingine kama vile kasino na odds za mechi kadha wa kadha.[6]

Ubashiri wa Mtandaoni

hariri

Licha ya kuendesha michezo ya kubashiri kwa mtandao, Meridian Bet Tanzania pia inaendesha michezo ya kasino ya mtandaoni na aina zingine za michezo ya kubashiri

===Huduma Katika Maeneo Maalumu===   Meridianbet ina mfumo kamilifu wa suluhisho la ubashiri katika maeneo maalumu ya maduka. Hii inafanya kazi kama eneo lililoandaliwa maalumu kwa ajili ya ubashiri salama katika maduka, huku kukiwa na mfumo salama wa uendeshaji, uongozi, ripoti na masuala ya kodi.

Programu ya Apple Watch

hariri

Meridian Bet ni waendeshaji wa michezo ya kubashiri wa kwanza kuwapa wateja wake huduma ya programu ya Apple Watch. Programu hii inawasaidia watumiaji kufahamu matokeo moja kwa moja, na kupata taarifa na kufurahia ubashiri moja kwa moja. Apple Watch imeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa kampuni wa iOS.

Sera za Ubashiri

hariri

Meridian Bet Tanzania ina sera makini za kubashiri kistaarabu ambazo zinatokana na misimamo tajwa hapa chini;

  • Kulinda dhidi ya uraibu wa michezo ya kubashiri
  • Kulinda watoto dhidi ya shughuli za ubashiri
  • Usalama wa wachezaji na makundi maalumu
  • Usalama wa mchezo

Huduma kwa Jamii

hariri

Kama Kampuni, Meridianbet Tanzania inaamini katika kusaidia na kuinua makundi mabalimbali nchini yenye uhitaji, na wamekuwa wakifanya hivyo. Katika kipindi cha janga la Virusi vya Corona, Meridianbet iliendelea kushirikiana jamii na kutoa faraja wa makundi maalumu.

Meridianbet Tazania imekuwa ikitoa misaada kwa kaya za vijijini[7], wagonjwa mabilimbali[8], hostpitali[9][10], waathirika wa madawa ya kulevya na makundi mengine muhimu[11][12]. Kampuni pia imekuwa ikiwasaidia wafanyakazi wake katika kuboresha maisha yao na maisha ya familia zao.

Ukuaji Kimataifa

hariri

Meridianbet imekuwa na rekodi nzuri ya kujitanua zaidi kuyafikia maeneo mapya moja kwa moja au kwa uwakilishi kupitia mfumo wake wa biashara. Meridianbet inatazama fursa za kufanya kazi na nchi zenye uthibiti na pale ambapo fursa za kutokuwepo udhibiti zinatokea.

Soma pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. madukani
  2. "mtandaoni". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-01. Iliwekwa mnamo 2020-07-24.
  3. "Bonasi ya 5% Unapojiunga na Meridian Bet Tanzania", globalpublishers.co.tz. Retrieved on 21 July 2020. 
  4. "Muongozo wa Kubashiri Afrika", africanbettingguide.com. Retrieved on 21 July 2020. Archived from the original on 2020-07-23. 
  5. "Meridianbet Tanzania Review 2021: Is Meridian Bet TZ reliable?". How to Bet on Football: Predictions & Betting Tips - Tccia.co.tz (kwa American English). 2020-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
  6. "Bonasi Kubwa ya TShs milioni 300 kutoka Meridian Bet Tanzania", soccerbet.co.tz. Retrieved on 21 July 2020. Archived from the original on 2020-07-23. 
  7. "MERIDIAN BET YAENDELEA KUTOA MSAADA KWA JAMII, WAOMBWA KUSAIDIA WALIO VIJIJINI - MTAA KWA MTAA BLOG". www.mtaakwamtaa.co.tz. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
  8. Michuzi Blog. "Meridian Bet yatoa msaada wa vifaa tiba kwa Wanaougua uti wa mgongo nchini". JIACHIE. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
  9. "Meridianbet Yamwaga Misaada Ocean Road Hospital (Picha +Video) - Global Publishers". globalpublishers.co.tz. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
  10. "Hospitali Ya Temeke Kuwa Na Vyumba Sita Vya Upasuaji - Global Publishers". globalpublishers.co.tz. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
  11. "Waathirika Dawa za Kulevya Waomba Elimu, Wapokea Msaada wa Meridian Bet - Global Publishers". globalpublishers.co.tz. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
  12. "Wenye Ualbino Watamani Kujiajiri - Global Publishers". globalpublishers.co.tz. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.

Kiungo cha nje

hariri