Methailskopolamini
Methailskopolamini (kwa Kiingereza: Methylscopolamine; pia inajulikana kama methskopolamini au methscopolamine), ni dawa iliyotumiwa kutibu vidonda vya tumbo.[1] Matumizi yake yamebadilishwa zaidi na vizuizi vya pampu ya protoni na vizuizi vya H2 ambavyo vinafaa zaidi.[1]
Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kinywa kikavu, kupunguka jasho, kuona giza, na kuongezeka kwa shinikizo la ndani ya macho.[1]"Methscopolamine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)</ref> Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio, kuhisi usingizi na kiharusi cha joto.[1] Ni antimuscarinic ambayo hufanya kazi kwa kuzuia asetilikolini. [1]
Methailskopolamini ilipewa hati miliki katika mwaka wa 1902 na kuidhinishwa kwa ajili ya matibabu mwaka wa 1947.[2] Nchini Marekani, vidonge 60 vya miligramu 2.5 hugharimu takriban Dola 32 kufikia mwaka wa 2021.[3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Methscopolamine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fischer J, Ganellin CR (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 446. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-15. Iliwekwa mnamo 2020-09-20.
- ↑ "Methscopolamine Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Methailskopolamini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |