Metras (aliuawa katikati ya karne ya 3) alikuwa mfiadini Mkristo wa Aleksandria (Misri) ambaye kwa kukataa kutamka maneno yasiyofaa aliuawa kwa kupigwa mawe wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Januari[1][2].

Pengine wanatajwa kama wafiadini wenzake Saturnini, Tirso, Vikta, Tarsisi, Zotiko na Siriaki[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.