Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania
Mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania (postikodi Tanzania) umeanzishwa tangu mwaka 2012. Msimbo wa posta ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nchini. Kila kata ina msimbo wa tarakimu tano.
Nia ni kuwa kila barua inayotumwa nchini Tanzania ionyeshe namba hiyo juu ya bahasha yake kama sehemu ya anwani ya barua au kifurushi ili kurahisisha na kuharakisha usafirishaji.
Namba ya msimbo wa posta ni tofauti na namba ya sanduku la posta; msimbo wa posta unahusu mahali au eneo, ilhali sanduku la posta linamhusu mpokeaji wa barua.
Muundo wa tarakimu katika msimbo wa posta wa Tanzania
Msimbo wa posta nchini Tanzania huwa na tarakimu tano zilizopangwa kufuatana na ngazi za utawala wa nchi:
- tarakimu ya kwanza inaonyesha kanda
- tarakimu ya pili (pamoja na inayotangulia) inaonyesha mkoa
- tarakimu ya tatu (pamoja na zinazotangulia) inaonyesha wilaya au halmashauri
- tarakimu za nne na tano (pamoja na zinazotangulia) zinaonyesha kata.
- Badala ya kata tarakimu kamili zinaweza kuteuliwa pia kwa ajili ya mteja mkubwa anayepokea barua nyingi sana, au eneo maarufu au shughuli maalumu. Mfano ni kampuni kubwa au wizara kuwa na msimbo wa pekee.
- Hakuna misimbo ya pekee kwa kata zote za Tanzania; wakati mwingine kata kadhaa za wilaya ileile zimeunganishwa kwa kazi ya posta na kuwa na msimbo mmoja[1]
- Badala ya kata tarakimu kamili zinaweza kuteuliwa pia kwa ajili ya mteja mkubwa anayepokea barua nyingi sana, au eneo maarufu au shughuli maalumu. Mfano ni kampuni kubwa au wizara kuwa na msimbo wa pekee.
Mfano:
6 5 4 0 1 ni msimbo wa posta kwa Kilwa Masoko.
• 6 ni tarakimu kwa Kanda ya Pwani
• 6 5 inaonyesha Mkoa wa Lindi
• 6 5 4 inataja Wilaya ya Kilwa (651 ni Lindi mjini, 563 Nachingwea, 655 Liwale, na kadhalika)
• Tarakimu za mwisho 0 1 ni za kata ya Kilwa Masoko.
Ilhali wilaya ya Kilwa huwa na kata 21, misimbo ya kata za Kilwa inaendelea kuanzia 6 5 4 0 1 (Kilwa Masoko) hadi 6 5 4 2 1 (Kibata).
Maana yake kama barua inaonyesha anwani ya „65421 Kibata“ inaweza kusafirishwa, si lazima mfanyakazi aulize Kibata iko wapi? Inatosha akijua ni barua kwenda pwani („6“) na Mkoa wa Lindi („65“). Pale Lindi wanajua wilaya zao na 654 ni Kilwa, vivyo hivyo hao wanajua kata katika eneo lao.
Utaratibu huo unatunza nafasi kwa kuanzishwa kwa vitengo vipya; kanda linaweza kuongezwa mikoa hadi 10, kila mkoa wilaya hadi 10, na kata hadi 100 kila wilaya. Kuna pia nafasi kwa kanda mpya 2.
Kanda
Kanda ni hizi zifuatazo, na kila mkoa wa Tanzania ni sehemu ya kanda fulani:
- Dar es Salaam (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, Kigamboni)
- Kaskazini
- Ziwa
- Kati
- Nyanda za Juu Kusini
- Pwani
- Zanzibar
Ugawaji wa misimbo ya posta kwenye mikoa na wilaya
1. Kanda ya Dar es Salaam
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Dar es Salaam | 11 | |
Manisipaa ya Ilala | 11, 12 | Kivukoni 11101 |
Manisipaa ya Kinondoni | 14 | Magomeni 14101 |
Manisipaa ya Temeke | 15 | Temeke 15101 |
Manisipaa ya Ubungo | 16 | Mburahati 16101 |
Manisipaa ya Kigamboni | 17 | Kimbiji 17101 |
2. Kanda ya Kazkazini
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Tanga | 21 | |
Mji wa Tanga | 211,
212 |
Central 21101
Tangasisi 21201 |
Wilaya ya Pangani | 213 | Bushiri 21307 |
Wilaya ya Muheza | 214 | Majengo 21401 |
Wilaya ya Mkinga | 215 | Daluni 21501 |
Mji wa Korogwe | 216 | Manundu 21601 |
Wilaya ya Korogwe | 216 | Mashewa 21627 |
Wilaya ya Lushoto | 217 | Sunga 21723 |
Wilaya ya Handeni | 218 | Kabuku 21815 |
Mji wa Handeni | 218 | Chanika 21801 |
Wilaya ya Kilindi | 219 | Songe 21901 |
Mkoa wa Arusha | 23 | |
Mji wa Arusha | 231 | Sekei 23101 |
Wilaya ya Arusha | 232 | Olturumet 23201 |
Wilaya ya Meru | 233 | Usa River 23301 |
Wilaya ya Monduli | 234 | Monduli Mjini 23401 |
Wilaya ya Longido | 235 | Longido 23501 |
Wilaya ya Karatu | 236 | Karatu 23601 |
Wilaya ya Ngorongoro | 237 | Orgosorok 23701 |
Mkoa wa Kilimanjaro | 25 | |
Manisipaa ya Moshi | 251 | Mawenzi 25101 |
Wilaya ya Moshi | 252 | Mabogini 25201 |
Wilaya ya Siha | 254 | |
Wilaya ya Hai | 253 | Machame Mashariki 25301 |
Wilaya ya Mwanga | 255 | Jipe 25501 |
Wilaya ya Same | 256 | Same 25601 |
Wilaya ya Rombo | 257 | Mahida 25701 |
Mkoa wa Manyara | 27 | |
Mji wa Babati | 271 | Babati 27101 |
Wilaya ya Babati | 272 | Magugu 27201 |
Wilaya ya Hanang | 273 | Katesh 27301 |
Wilaya ya Mbulu | 274 | Ayomohe 27401 |
Wilaya ya Kiteto | 275 | Kibaya 27501 |
Wilaya ya Simanjiro | 276 | Orkesumet 27601 |
3. Kanda ya Ziwa
4. Kanda ya Kati
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Dodoma | 41 | |
Manisipaa ya Dodoma | 411 ,
412 |
Tambukareli 41104
Makutopora 41201 |
Wilaya ya Bahi | 413 | Bahi 41301 Bahi Sokoni |
Wilaya ya Chamwino | 414 | Chilonwa 41401 |
Wilaya ya Kongwa | 415 | Kongwa 41501 |
Wilaya ya Mpwapwa | 416 | Mpwapwa mjini 41601 |
Wilaya ya Kondoa | 417 | Kondoa mjini 41701 |
Wilaya ya Chemba | 418 | Chemba 41801 |
Mkoa wa Singida | 43 | |
Manisipaa ya Singida | 431 | |
Wilaya ya Singida Vijijini | 432 | |
Wilaya ya Iramba | 433 | Kiomboi 43301 |
Wilaya ya Manyoni | 434 | Manyoni Urban 43401 |
Wilaya ya Mkalama | 435 | Kinyangiri 43501 |
Wilaya ya Ikungi | 436 | Ihanja 43601 |
Mkoa wa Tabora | 45 | |
Manisipaa ya Tabora | 451 | |
Wilaya ya Uyui | 452 | Goweko 45201 |
Wilaya ya Sikonge | 453 | Sikonge 45301 |
Wilaya ya Nzega | 454 | Nzega mjini 45401 |
Wilaya ya Urambo | 455 | Urambo 45501 |
Wilaya ya Igunga | 456 | Igunga 45601 |
Wilaya ya Kaliua | 457 | Kaliua 45701 |
Mkoa wa Kigoma | 47 | |
Manisipaa ya Kigoma-Ujiji | 471 | |
Wilaya ya Kigoma Vijijini | 472 | |
Mji wa Kasulu | 473 | |
Wilaya ya Kasulu | 473 | Kasulu Mjini 47301 |
Wilaya ya Kibondo | 474 | Kibondo Mjini 47401 |
Wilaya ya Buhigwe | 475 | Buhigwe 47501 |
Wilaya ya Uvinza | 476 | Uvinza 47601 |
Wilaya ya Kakonko | 477 | Nyabibuye 47709 |
5. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
6. Kanda ya Pwani
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Pwani | 61 | |
Mji wa Kibaha | 611 | Mailimoja 61102 |
Wilaya ya Kibaha | 612 | Mlandizi 61201 |
Wilaya ya Bagamoyo | 613 | Yombo 61306 |
Wilaya ya Kisarawe | 614 | |
Wilaya ya Mkuranga | 615 | Kiparang'anda 61502 |
Wilaya ya Rufiji Wilaya ya Kibiti |
616 | Utete 61601 Kibiti 61610 |
Wilaya ya Mafia | 617 | |
Mkoa wa Mtwara | 63 | |
Manisipaa ya Mtwara | 631 | |
Wilaya ya Mtwara | 632 | |
Wilaya ya Tandahimba | 633 | |
Wilaya ya Newala | 634 | |
Wilaya ya Masasi | 635 | Mwenge Mtapika 63529 |
Wilaya ya Nanyumbu | 636 | Nangomba 63601 |
Mkoa wa Lindi | 65 | |
Manisipaa ya Lindi | 651 | Makonde 65101 |
Wilaya ya Lindi | 652 | Nachunyu 65201 |
Wilaya ya Nachingwea | 653 | |
Wilaya ya Kilwa | 654 | Kilwa Masoko 65401 |
Wilaya ya Liwale | 655 | Liwale Mjini 65501 |
Wilaya ya Ruangwa | 656 | Ruangwa 65601 |
Mkoa wa Morogoro | 67 | |
Manisipaa ya Morogoro | 671 | |
Wilaya ya Morogoro | 672 | |
Wilaya ya Mvomero | 673 | |
Wilaya ya Kilosa | 674 | |
Wilaya ya Kilombero | 675 | |
Wilaya ya Ulanga | 676 | Mahenge 67601 |
Wilaya ya Gairo | 677 | Gairo 67701 |
7. Kanda ya Zanzibar
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja | 71 | |
Wilaya ya Mjini | 711 | |
Wilaya ya Magharibi Unguja | 712 | Mwanakwerekwe 71201 |
Mkoa wa Kusini Unguja | 72 | |
Wilaya ya Kusini | 721 | |
Wilaya ya Kati | 722 | Dunga 72201 |
Mkoa wa Kaskazini Unguja | 73 | |
Wilaya ya Kaskazini A | 731 | |
Wilaya ya Kaskazini B | 732 | Mahonda 73201 |
Mkoa wa Kusini Pemba | 74 | |
Wilaya ya Mkoani | 741 | |
Wilaya ya Chake Chake | 742 | Chanjaani 74201 |
Mkoa wa Kaskazini Pemba | 75 | |
Wilaya ya Wete | 751 | |
Wilaya ya Micheweni | 752 | Micheweni 75201 |
Tanbihi
- ↑ Kwa mfano wilaya za Handeni mjini na vijijini ziko pamoja chini ya na. 218; ilhali kila kata ya wilaya ya Handeni vijijini ina msimbo wa posta, upande wa mjini kuna misimbo 3 pekee ilhali kata za mjini ziko 12.