Michaela bryde
Michaela Blyde ( alizaliwa Disemba 29, 1995) ni mchezaji wa raga ya wachezaji saba wa kulipwa wa New Zealand na mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki. Mnamo 2018, alishinda medali za dhahabu katika Michezo ya Jumuiya ya Madola na Kombe la Dunia la Raga ya wachezaji Saba.
Blyde aliichezea New Zealand kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17 kwenye mashindano ya ubingwa kwa wanawake ya Oceania.[1]
Alikuwa mfungaji bora wa majaribio kwenye mashindano ya Raga ya Wanawake kwa wachezaji saba msimu wa 2016-17, na alitawazwa kuwa Mchezaji Bora wa mwaka wa Raga ya Wanawake kwa wachezaji saba Duniani mwaka 2017.[2][3] Mwaka 2018, Blyde alitawazwa Mchezaji Bora wa Dunia wa Raga ya Wanawake wa Saba kwa mwaka wa pili mfululizo.[4]
Marejeo
hariri- ↑ "Taranaki's Michaela Blyde in Sevens heaven". Stuff (kwa Kiingereza). 2013-10-03. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.
- ↑ "Michaela Blyde reaches her goals and some". Stuff (kwa Kiingereza). 2017-07-05. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.
- ↑ "New Zealand dominates World Rugby Awards". RNZ (kwa New Zealand English). 2017-11-27. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.
- ↑ "World Rugby Awards: Michaela Blyde best sevens player for second successive year". Stuff (kwa Kiingereza). 2018-11-26. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.