Mukhethwa Mukhadi (alizaliwa mnamo tarehe 22 Juni 1997), anajulikana kwa taaluma yake kama Mike Tuney, ni mwimbaji wa nyimbo za rapu, mkurugenzi na mtayarishaji wa rekodi nchini Afrika Kusini. Anajulikana kwa wimbo wake wa "Secure the Bag" na alipata umaarufu baada ya wimbo wake "Tonight" kusambaa mnamo mwaka 2016.[1]

huyu ni rapper wa afrika kusini

Maisha ya awali

hariri

Mukhadi alizaliwa na kukulia katika kijiji kidogo kiitwacho Sendedza, kilicho nje kidogo ya Thohoyandou huko Limpopo. Upendo[2] wake kwa hip hop ulianza akiwa na umri wa miaka (12 )tu na baada ya miaka michache, alianza kuandika na kurekodi nyimbo zake mwenyewe.[3]

Kazi ya muziki

hariri

Baada ya kuachia mixtape mbili na igizo moja lililorefushwa, Mike alitoa albamu yake ya kwanza kabisa katika siku yake ya kuzaliwa ya 23 mwaka wa 2020[4], inayoitwa "I Wish I Could". Alipata kutambuliwa baada ya kuachia mixtape yake ya kwanza inayoitwa "X-Pectations" mwaka wa 2016. Mike Tuney alitoa wimbo wake wa kwanza aliojitayarisha uitwao "Mama I'm Sorry" akimshirikisha Vhole mnamo 2019, wimbo huo pia ulionekana kwenye albamu yake ya 2020.[5]

Marejeo

hariri
  1. https://www.zoutnet.co.za/articles/entertainment/50188/2019-06-08/who-is-mike-tuney-
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-01-12. Iliwekwa mnamo 2022-04-25.
  3. https://www.zoutnet.co.za/articles/entertainment/50188/2019-06-08/who-is-mike-tuney-
  4. https://medium.com/@violadeen/mike-tuney-drops-his-first-album-436602a16115
  5. https://www.zoutnet.co.za/articles/entertainment/50188/2019-06-08/who-is-mike-tuney-
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mike Tuney kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.