Mkutano huria
(Elekezwa kutoka Mikutano huria)
Mkutano huria ni mkutano ambao unaendeshwa na wahudhuriaji au wajumbe badala ya mwandaaji au waandaaji wa mkutano. Katika mkutano wa aina hii hakuna watoa mada na wapokea mada, hakuna watoa hotuba na wasikilizaji. Wahudhuriaji wote ndio watoa mada na wapokea mada. Dhana hii imepewa umaarufu na wataalamu wawili wa programu ya tarakilishi, Lenn Pryyor na Dave Winer.