Atlas (milima)

(Elekezwa kutoka Milima ya Atlas)
Safu za milima ya Atlas.

Milima ya Atlas (kwa Kiberber: Idurar n Watlas, kwa Kiarabu: جبال الأطلس‎) ni safu ya milima kunjamano katika Afrika ya kaskazini-magharibi. Ina urefu wa takriban kilomita 2,400 kuanzia Moroko kwa kuvukia Algeria hadi Tunisia. Milima ya Atlas hutenganisha pwani ya Atlantiki na Mediteranea kutoka jangwa la Sahara.

Mwinuko wa juu ni Jebel Toubkal nchini Moroko inayofikia mita 4,167 juu ya UB.

Wakazi wa milima hii ni hasa makabila ya Waberber.

Jina la milima hii linatokana na mmoja wa miungu ya Ugiriki ya Kale, Atlas.

AsiliEdit

Atlas ni milima kunjamano yaani tokeo la kugongana kwa mabamba ya gandunia ya Afrika na Ulaya kulikosababisha kukunjwa kwa uso wa ardhi na kutokea kwa safu za milima hii. Mchakato huu ulitokea mara mbili. Mara ya kwanza takriban miaka milioni 300 iliyopita, wakati bamba la Amerika Kaskazini liligongana na bamba la Afrika na tokeo lake ni safu ya Antiatlas katika Moroko ya kusini. Lakini sehemu kubwa ya Atlas ilitokea kutokana na mgongano wa mabamba ya Afrika na Ulaya katika kipindi cha miaka milioni 65 - 2 iliyopita.[1][2]

Kutokana na historia hii kuna hatari ya mtetemeko wa ardhi katika eneo la Atlas na miji kadhaa iliwahi kuharibiwa.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  1. UAB.es Potential field modelling of the Atlas lithosphere
  2. UAB.es Crustal structure under the central High Atlas Mountains (Morocco) from geological and gravity data, P. Ayarza, et al., 2005, Tectonophysics, 400, 67-84