Minou ni jina la kutaja wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Marquis Original kati ya miaka ya tisini. Wimbo ulitolewa mwaka wa 1992. Mashairi yake anamsihi mke wake wasiachana na kuwambia abadili uamuzi wake kwa amemzoea sana. Pamoja na kulazimisha talaka, bado bibie aliendelea kumtangazia mbovu mitaani. Anamuonea huruma kwa wale waliomdanganya wamemkimbia na wamemwacha mtu hana hata pa kushikia.

"Minou"
Wimbo wa Orchestra Marquis Original
Umetolewa 1992
Umerekodiwa 1992
Aina ya wimbo Muziki wa dansi
Lugha Kiswahili
Urefu 8:13
Mtunzi Tshimanga Assossa
Mtayarishaji Tshimanga Assossa

UchambuziEdit

MashairiEdit

Wewe ndiyo uliyoanza..
kunitaka eti tuachane..
Nilikubembeleza usiku kucha..
Ubadilishe uamuzi wako mama..
Nimekuzoea eeeh..
Hukutaka kunisikia..
Ukanihukumu bila hatia..
Ukanitangazia ubaya ulivyotaka.. We Minou eeh.. We Minou eeh..
Ona sasa wivu wako...
Mwenzako mie masikini..
Nilijua eeeh..
Waliokudanganya wapo wapi....
Wamekuacha huna pa kuanzia....
Dunia ya leo matata...
We Minou eeh..
We Minou eeh..

WahusikaEdit

  • Mtunzi: Tshamanga Kalala Asossa
  • Waimbaji: Tshimanga Asossa, Bobo Sukari, Freditto Butamu (marehemu) Mutombo Lufungula 'Audax' (marehemu) Mukumbule Lolembo 'Parash'.
  • Mpiga solo: Kivukutu Moto na Tchacho.
  • Besi: Ilunga Banza ' Mchafu'. (marehemu)
  • Mpiga rhythim: Mulenga Kalonji 'Vata' (marehemu)
  • Saxa: Berry Kankonde (marehemu)
  • Tarumbeta: Kaumba Kalemba (marehemu)
  • Ngoy Mubenga.
  • Keyboard: Mbuya Makonga 'Adios'.
  • Ngoma: Mharami Seseme

Tazama piaEdit

Viungo vya NjeEdit