Mirèio ni kazi ya fasihi ya kishairi iliyoandikwa na Frédéric Mistral miaka ya 1851-1858 na kutolewa 1859. Ni kazi yake ya kwanza tena maarufu kabisa. Dhamira yake ni upendo baina binti mmoja na kijana. Mistral aliiandika kazi hiyo kwa lugha ya Kioksitani akitunga nyimbo kuminambili. Kila wimbo una beti zenye michororo saba, kama katika mashairi ya kimapokeo ya Ufaransa wa Kusini. Shairi la Mirèio limekuwa mfano hodari kwa maisha na utamaduni wa eneo hilo zima.

Mirèio
Mirèio

Mkondo wa hadithi hariri

Mirèio ni binti wa Ramoun, mtajiri kule Ufaransa wa Kusini. Vincèn, mfanyakazi mzururaji, hufika nyumbani kwake Mirèio, nao wanagundua kwamba wanapendana. Ndiyo sababu Mirèio anakataa wanaume wengine ambao wamechaguliwa na baba yake. Mmojawao, jina lake Ourias, anapigana naye Vincèn na kumwumia vibaya. Mirèio anamwuguza Vincèn lakini Ramoun anaendelea kukataa uhusiano baina hao wawili. Hatimaye, Mirèio anakwenda hija kule Les Saintes Maries de la Mer ambako anafariki mbele za Vincèn na wazazi wake. Watakatifu hufika ili waelekeze nafsi yake Mirèio hadi mbinguni.

Marejeo hariri

  • (de) "Kindlers Literaturlexikon", Juzuu 7, 1970, Zürich, uk. 6339.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mirèio kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.