Misitu ya Chilapata

Msitu wa Chilapata ni msitu mnene uliopo karibu na mbuga ya wanyama ya Jaldapara huko Dooars, wilaya ya Alipurduar, Bengal Magharibi nchini India. Ina umbali wa kilometa 40 kutoka Alipurduar, na dakika chache kutoka mji wa Hasimara.

Ekolojia

hariri

Msitu unatengeneza njia ya tembo kati ya mbuga ya wanyama ya Jaldapara na hifadhi ya simbamarara Buxa[1]. Aina mpya za wanyama zinaendelea kugundulika[2]. Msitu ulikuwa makazi ya idadi kubwa ya vifaru.

Inatarajiwa kwamba utalii wa mazingira utaleta vyanzo vipya vya mapato kwa wazawa wa Rabha, ambao kwa sasa wanategemea msitu kwa mahitaji ya kuni.

Marejeo

hariri