Kigezo:Infobox medical intervention Misukumo ya tumbo, pia inajulikana kama mbinu ya Heimlich, ni matibabu ya kukabwa sana (kuziba kwa njia ya hewa kutokana na kitu cha kigeni).[1] Inatumika hasa kwa wale walio na umri wa zaidi ya mwaka mmoja ambao hawawezi kukohoa lakini wanaendelea kuwa na ufahamu.[2] Haipendekezi kwa wale walio chini ya mwaka mmoja au ambao ni wajawazito.[3] Katika wale walio chini ya mwaka mmoja, kupigwa kwa nyuma (mgongoni) na kusukumwa kwenye kifua kunapendekezwa, wakati kwa wale ambao ni wajawazito kusukumwa kwenyr kifua hutumiwa.[2][1]

Mwokoaji anapaswa kuanza kwa kusimama nyuma ya mtu aliyeathirika.[3] Kiisha wanapaswa kuifunga mikono yao kiunoni mwa mtu huyo na kuiinamisha mbele.[1][3] Hii inafuatwa na kukunja mkono mmoja uwe kama ngumi, juu kidogo ya kitovu cha tumbo, na kuutumia mkono mwingine na sehemu ya juu ya mikono kuvuta ngumi hiyo kuelekea ndani na juu.[3] Harakati hii ya mwisho inaweza kurudiwa mara tano hadi kumi.[1][3] Kwa mtoto, mtu anaweza kuhitaji kupiga magoti.[1]

Matatizo yake yanaweza kujumuisha jeraha la mbavu, ini, tumbo au wengu.[1] Inawezekana kwamba kutapika kunaweza pia kutokea.[1] Ikiwa mtu atapoteza fahamu, ufufuaji wa moyo na mapafu (CPR) unapaswa kuanza.[1] Henry Heimlich, daktari wa upasuaji wa Marekani, anasifika kwamba ndiye wa kwanza kuunda taratibu hizi katika mwaka wa 1974.[4]

Marejeleo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Mer2022Pro
  2. 2.0 2.1 Duckett, Stephanie A.; Bartman, Marc; Roten, Ryan A. (2022). "Choking". StatPearls. StatPearls Publishing. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 22 Aprili 2022.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "What should I do if someone is choking?". nhs.uk (kwa Kiingereza). 26 Juni 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Machi 2022. Iliwekwa mnamo 23 Aprili 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"What should I do if someone is choking?". nhs.uk. 26 June 2018. Archived from the original on 23 March 2022. Retrieved 23 April 2022.
  4. "Dr Henry Heimlich uses Heimlich manoeuvre to save a life at 96". (en)