Mjasiriamali

Mjasiriamali ni mtu ambaye anaandaa, anapanga au anasimamia biashara fulani, akikubali kukabiliana na hatari za kibiashara zinazoweza kujitokeza ilhali analenga kupata faida.[1]

Mjasiriamali nchini Pakistani

Mjasiriamali mara nyingi huonekana kama mbunifu, chanzo cha mawazo anzilishi, mwenye kuvumbua bidhaa au huduma mpya na biashara. Pia mjasiriamali ni mtu anayeweza kusaidia sana maendeleo ya kiuchumi nchini mwake, ndiyo maana nchi tajiri zaidi duniani zina wajasiriamali wengi na mashuhuri sana, yaani, ujasiriamali unaonekana kama lazima kwa uboreshaji wa hali ya kiuchumi katika nchi yoyote. [2]

Mjasiriamali huwa na jukumu muhimu katika uchumi wowote, kwa kutumia ustadi wa kijasiriamali na kuleta maoni mazuri katika soko.[3]

MarejeoEdit

  1. entrepreneurship.html entrepreneurship Archived 16 Novemba 2018 at the Wayback Machine., Tovuti ya Businessdictionary.com, iliangaliwa Agosti 2020
  2. Adam Hayes. What You Should Know About Entrepreneurs (en). Investopedia. Iliwekwa mnamo 2020-02-13.
  3. Adam Hayes. What You Should Know About Entrepreneurs (en). Investopedia. Iliwekwa mnamo 2020-02-13.
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mjasiriamali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.