Koma

(Elekezwa kutoka Mkato)

Koma au mkato (,) ni alama ya uakifishaji. Inakaa kwenye mstari wa kuandika ikiwa na umbo la nukta yenye mkia wa kupinda unaelekea chini au alama ya 9 ndogo ambako nafasi imejazwa, wakati mwingine pia kama mstari mfupi inayonama.

Koma au mkato

Wakati wa kusoma ina kituo kifupi, au kutenganisha maneno yanayoorodheshwa.

Kazi yake ni kutenganisha sehemu tofauti ndani ya sentensi.

Wakati wa kuandika namba inaweza kutumiwa

  • kama alama desimali inayotenganisha namba halisi na sehemu ambazo ni ndogo kuliko 1
  • au kama alama ya kutenganisha elfu, mfano 1,000 (elfu moja) - 10,000 (kumi elfu) - 1,000,000 (milioni)

Matumizi ni tofauti kati ya nchi na nchi. Mkutano mkuu wa Ofisi ya Kimataifa ya Vipimo uliamua mwaka 2003 kukubali matumizi ya ama nukta au koma kuwa alama ya desimali. [1]

Mara nyingi nchi zinazotumia Kiingereza hutumia koma kuwa alama ya desimali, na hivyo nukta kuwa kitenganishi elfu.

  1. [1], Resolution 10.