Mkoa wa Pangani (DOA)

Mkoa wa Pangani ilikuwa mkoa mmoja kati ya mikoa 21 ya koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (DOA, Deutsch Ostafrika) iliyokuwa mtangulizi wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi wa leo.

Eneo na mipaka hariri

 
Mkoa wa kihistoria wa Pangani (DOA) mnamo 1913 (na. III)
 
Pangani 1913

Mkoa huu ulikuwa na eneo la kilomita za mraba 12,600 kwa hiyo ilikuwa kati ya mikoa midogo zaidi ya koloni hii. Makao makuu (jer. Bezirksamt) yalikuwepo Pangani mjini.

Mkoa huu ulipakana na

Mkoa huu ulikuwa na ofisi ndogo (jer. Bezirksnebenstelle) pale Handeni.

Wakazi hariri

Mwaka 1913 kulikuwa na wakazi Waafrika 98,500, pamoja na 1,814 Waasia (Wahindi, Waarabu hasa) na Wazungu 123. Katika idadi ya Waafrika kulikuwa na wafanyakazi 6,000 kutoka nje ya mkoa kwenye mashamba makubwa ya kibiashara waliofika hapa kwa kutafuta ajira.

Mji wa Pangani ulikuwa na wakazi 3,000, kati yao Waarabu 400 na Wahindi 400. Iliwahi kuwa mji muhimu zaidi ya pwani baina ya Mombasa na Bagamoyo lakini biashara yake ilihamia polepole Tanga iliyokuwa na bandari nzuri iliyofaa kwa meli kubwa.

Uchumi hariri

Kabla ya ukoloni wafanyabiashara Waarabu na Waswahili walianzisha mashamba ya sukari katika mazingira ya Pangani yaliyolimwa na watumwa wao. Abushiri bin Salim aliyeanzisha vita dhidi ya Wajerumani mwaka 1889 alikuwa mmoja ya wajasiriamali Waarabu wa eneo la Pangani. Lakini baada ya miaka ya kwanza ya ukoloni utumwa ulikomeshwa na mashamba ya sukari yaliporomoka.

Badala yao mashamba makubwa ya makampuni na walowezi Wazungu yalianza kuenea (mwaka 1913 makampuni 7 na walowezi 13). Kikogwe-Mwera (leo: kata ya Mwera (Pangani) ilikuwa shamba la Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki na sehemu ya kwanza ambako mikonge ililimwa katika Afrika ya Mashariki. Mashamba yaliyotumiwa na Wazungu yalikuwa na kilomita za mraba 436, ilhali kiasi kikubwa ilikodishwa na serikali ya kikoloni kwa walowezi na sehemu ndogo tu kuuzwa. Pamoja na mikonge mashamba haya yalikuwa pia na kahawa na minazi.

Kwenye mwaka 1913 takwimu ya Kijerumani ilihesabu ng'ombe 57,860, kondoo 41,070, mbuzi 48,575 na punda 1218. Karibu mifugo yote ilikuwa mali ya Waafrika, Wazunga wa eneo hili hawakufuga.

Mji na bandari ya Pangani hariri

Pangani yenyewe iliwahi kuwa mji muhimu wa Waswahili kabla ya ukoloni maana ilikuwa bandari kuu ya kutazama kisiwa cha Pemba. Mji uko kwenye mdomo mpana wa mto Pangani na huu mdomo ulikuwa bandari salama kwa mashua na jahazi ndogo. Ila tu meli hazikuweza kuingia zilipaswa kukaa mbali kiasi na ufuko na kupokea au kutoa mizigo na abiia kwa msaada wa maboti madogo.

Mwaka 1908 zilifika meli 79 na jahazi 318. Thamani ya bidhaa zilizofika Pangani mwaka 1912 ilikuwa mark milioni 1.002, thamani ya bidhaa zilizotumwa ilikuwa mark milioni 1.923, ndani ya jumla hii katani kwa mak milioni 1.7.

Marejeo hariri