Mnavunavu
(Physalis peruviana )
Mnavunavu
Mnavunavu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Solanales (Mimea kama mnavu)
Familia: Solanaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mnavu)
Jenasi: Physalis
Spishi: P. peruviana
L.

Mnavunavu au mzabibu-bata (Physalis peruviana) ni mmea au kichaka katika familia Solanaceae ambao unapanda mara nyingi juu ya mimea mingine au egemeo lolote. Matunda yake yalikayo huitwa manavunavu. Kaliksi, ambayo imeunda na sepali, izungashia tunda kama kibofu. Kama tunda likiiva, kaliksi inakauka. Tunda bivu lina rangi ya manjano na ladha maalum tamu. Asili ya mnavunavu ni Peru, Kolombia na Ekuador lakini sasa hupandwa Afrika ya Kusini na Mashariki, Australia, Nyuzilandi na visiwa kadhaa vya Pasifiki.

Picha hariri

  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mnavunavu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.