Moïse Katumbi

Mwanasiasa wa Kongo (DRC)

Moïse Katumbi Chapwe (alizaliwa 28 Desemba 1964) ni mwanasiasa na mfanyabiashara wa Kongo.[1]

Moïse Katumbi

Alikuwa Gavana wa Mkoa wa Katanga, eneo la kusini mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kuanzia 2007 hadi Septemba 2015.[2]

Alikuwa pia mwanachama wa Chama cha Watu cha Mageuzi na Demokrasia (PPRD) hadi 29 Septemba 2015.[3]

Ametajwa kama "labda mtu wa pili mwenye mamlaka zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya rais, Joseph Kabila"[4] na alipewa na Jeune Afrique jina "African Personality of 2015".[5]

Mnamo Desemba 2021, Moïse Katumbi alizindua rasmi chama chake cha kisiasa kwa kuzingatia uchaguzi wa rais wa 2023.

Maisha

hariri

Moïse Katumbi alizaliwa na mama Mkongo na baba Mgiriki, Nissim Soriano, aliyetorokea Rhodes kati ya vita viwili vya dunia ilipotawaliwa na Italia ya Kifashisti.[6] Alihamia Katanga, karibu na Ziwa Moero.[7] kulingana na matamko kadhaa kutoka kambi ya rais, Moïse Katumbi angeshikilia uraia wa Zambia.[8]

Moïse Katumbi amemwoa Carine Katumbi na kupata watoto ambao ni Ariel, Nissin, Lael, Ishmael, Jonathan na Champion.[9]

Moïse Katumbi alisomea shule ya Kiwele huko Lubumbashi na misheni ya Kapolowe alipopata stashahada (diploma) ya Jimbo, na kuhitimu katika saikolojia.[10]

Wakati alipokuwa akisimamia biashara ya kaka yake na kuanzisha shughuli nyingine nchini Zambia, alijifunza Kiingereza na kuhudhuria madarasa ya usimamizi.[11]

Biashara

hariri

Biashara ya uvuvi

hariri

Moïse Katumbi alianza kazi yake ya biashara kwa kuuza samaki shuleni akipata faida ya kwanza ya dola 40 katika umri wa miaka 13.[12] Kisha alistawi katika biashara ya uvuvi katika Ziwa Moero akisambazia kampuni ya madini inayomilikiwa na serikali, Gécamines.[13]

Etablissement Katumbi

hariri

Ameanzisha shughuli na kubadilisha kwa kasi kwenye sekta nyingine: usafiri, biashara, usambazaji wa vyakula.[14] Kutoka kwenye mfumo wa mtandao mkubwa wa barabara yenye maelfu ya kilomita hadi usambazaji umeme vijijini na mijini, utengenezaji na ukarabati wa shule na hospitali, Katumbi ameacha nyayo zake katika Mkoa mzima wa Katanga.[15]

Mwaka wa 1987, alifanya Etablissement Katumbi kujumuisha shughuli zake zote kuwa sehemu za madini, usafiri na usambazaji wa vyakula.[16]

Kampuni ya Madini ya Katanga

hariri

Miaka kumi baadaye, baada ya kipindi cha mabadiliko, aliunda MCK (Kampuni ya Madini ya Katanga), ambayo ilirejesha shughuli za kuchimba madini ya shaba na kobalti kwa 80% Gécamines.[11] Novemba 9, 2015, kampuni ya Ufaransa Necotrans ilinunua MCK kwa kiasi cha pesa ambacho hakikutajwa.[17][18]

Kandanda

hariri

TP Mazembe

hariri

Tangu 1997, Moïse Katumbi pia ni Mwenyekiti wa timu ya kandanda TP Mazembe mjini Lubumbashi.[19] Timu imeshinda mara tano Ligi ya Mabingwa ya CAF pamoja na mafanikio ya mwisho mwaka wa 2009,[20] 2010,[21] na 2015.[22] Pia imecheza fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu ya FIFA mwaka wa 2010 huko Abu Dhabi.[23] na 2015 jijini Tokyo.[24]

Kilabu kiliandikisha historia kwa kuwa kilabu cha kwanza kutoka Afrika kwa kupita ngome ya Ulaya na Amerika Kusini, kufika finali ya Kombe la Dunia ya Vilabu ya FIFA, ambapo kilishindwa na Inter Milan.[25]

Moise Katumbi pia alianzisha kandanda kama mpango wa jamii ili kushirikisha na kufunza vijana katika mkoa wa Katanga. (Zaidi ya wanachama 2'000 kufikia sasa) Katumbi pia alikamilisha uwanja wa TP Mazembe mwaka wa 2011 kwa gharama ya dola milioni 35.[22]

Tume ya Mikakati ya FIFA

hariri

Tangu Januari 2, 2012, alichaguliwa kwenye tume ya Mikakati ya FIFA.[26][27]

Maisha ya siasa

hariri

Mwaka wa 2006 na 2011, Moïse Katumbi alisaidia kampeni za Joseph Kabila kuwania Urais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.[28] Hata hivyo, kama wengine wengi, Katumbi alijitenga hadharani na Kabila mwaka wa 2015.[29]

Katika makala ya Reuters yaliyochapishwa Novemba 13, 2015, Moïse Katumbi alipendekeza kinga dhidi ya kushtakiwa kwa Kabila baada ya kuondoka afisini "kama jaribio la kumshawishi Kabila kuondoka afisini wakati ambapo muhula wake wa pili na wa mwisho kuchaguliwa kukamilika mwaka unaofuatia". Moise aliongeza kuwa Kabila kuondoka kwa mujibu wa muda wa katiba kutamfanya kuwa "baba wa demokrasia ya Kongo" na rais wa kushukuriwa na Wakongo.[30][31][32]

Makamu wa Bunge la Taifa

hariri

Mwaka wa 2006, alichaguliwa kuwa Makamu katika Bunge la Taifa kabla ya kuchaguliwa Gavana wa Mkoa wa Katanga Januari 2007, kwa kupokea kura 94 kati ya 102.[33]

Gavana wa Katanga

hariri

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka akiwa Gavana wa Katanga, Moïse Katumbi alitekeleza marufuku ya uhamishaji wa madini ghafi, hivyo kulazimisha kampuni kubwa za kuchimba madini kujenga mageuzi katika mkoa.[34] Aliongeza ushuru wa ndani kutoka dola bilioni 3 kwa kupambana na ufisadi na kuongeza uuzaji wa nje wa shaba. Mapato haya alitumiwa kujenga shule, barabara, hospitali, na kulea maji safi (kutoka asilimia 3 hadi 67 ya ufikiaji wa maji safi) kwa watu wengi maskini.[33]

Kufuatia data ya madini ya Chamber, Moise Katumbi aliongeza uzalishaji wa shaba kutoka tani 8'000 mwaka wa 2006 hadi zaidi ya tani milioni 1 mwaka wa 2014. Utawala wake pia umejenga zaidi wa barabara zenye urefu wa kilomita 1'000 na kupunguza bei ya unga wa mahindi kutoka dola 45 hadi dola 10 kwa kila gunia.[35]

Mwaka wa 2013, kufuatia Katiba ya Jimbo la nchi yake, Moïse Katumbi alitangaza kuwa asingegombea kwa muhula wa pili akiwa Gavana. Kwa uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2016, wachunguzi wengi wa taifa na kimataifa wanamwona kama mgombea mwenye nafasi na mrithi wa Joseph Kabila.[36][37][38]

Front Citoyen 2016

hariri

Mnamo 29 Septemba 2015 alijiuzulu kuwa Gavana, baada ya viongozi wa vyama saba vya siasa walipofurushwa kutoka kwenye Upande wa Wengi wa Urais kwa kuandika barua kwa Kabila ambapo waliuliza nia yake ya kujiondoa mwisho wa muhula wake wa pili mwaka wa 2016.[39][40] Katumbi aliongeza kuwa kujiuzulu kwake kutoka kwenye People's Party for Reconstruction and Democracy kungalimruhusu kuangazia majaribio ya serikali ya taifa kukiuka katiba na kuchelewesha uchaguzi[29] na pia kupata uhuru wake wa kuongea na kuchukua hatua.[41] Katika azimio lilo hilo, alitangaza kuwa ushauri muhimu miongoni mwa wanachama wa mashirika ya raia ungalifanyika ili kuunda vuguvugu la jamhuri na demokrasia nchini. Mnamo 19 Desemba 2015, Moïse Katumbi alijiunga na watu wengine mashuhuri wa Kongo katika muungano ulioitwa "Front Citoyen 2016". Chombo hiki kinajishughulisha na kulinda Katiba na kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka wa 2016 unafanyika.[42]

Mnamo Desemba 15, 2012, Wakfu wa Millenium Excellence ulimtuza Katumbi tuzo ya « Black Star of Africa 2012 » jijini Nairobi, Kenya. Tuzo ilitambua mafanikio yake na wajibu wake kama bingwa katika uongozi bora wa Afrika.[43]

Januari 2015, Moise Katumbi pia alipokea tuzo ya « Kiongozi wa Kandanda wa Mwaka » kutoka Shirikisho la Kandanda la Afrika.[44]

Mnamo Desemba 22, 2015, Moïse Katumbi alipewa jina « African Personality of 2015 » na Jeune Afrique, jarida kubwa la Afrika.[5]

Marejeo

hariri
  1. "Moïse Katumbi Chapwe Millenium Excellence Foundation". Millenium Excellence Foundation Africa. 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-03. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  2. Provinces of Congo (Kinshasa)
  3. "Is Katumbi's resignation a game changer in DRC?". Democracy in Africa. 21 Oktoba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "An old ally of Joseph Kabila leaves the ruling party", The Economist, 6 October 2015. Retrieved on 12 October 2015. 
  5. 5.0 5.1 "Sondage : Moïse Katumbi, Africain de 2015 selon les lecteurs de J.A., devant Mbonimpa et Mukwege - JeuneAfrique.com". JeuneAfrique.com (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2015-12-23.
  6. "Moise Katumbi Chapwe: The People's governor". Transterramedia. 10 Septemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-22. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Moïse Katumbi, un ovni en politique". Blog Le Soir. 31 Machi 2009.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Afrique Élections en RDC: nouvelle polémique sur la nationalité de l'opposant Moïse Katumbi". Radio France Internationale. 07 December 2023. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); line feed character in |title= at position 8 (help)
  9. "Matata III: M.Katumbi pas d'accord avec J. Kabila sur le choix d'un ministre". 7 sur 7. 28 Septemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-05. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Portrait de Moise Katumbi Chapwe". Enews 24. 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-17. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  11. 11.0 11.1 "La conscience - Moïse Katumbi : l'homme, son parcours et ses œuvres". www.laconscience.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-11-10. Iliwekwa mnamo 2015-09-16.
  12. "Moïse Katumbi Chapwe: A man the west would love to do business with". Forbes Custom.
  13. "Katanga Big Boss". Iliwekwa mnamo 2015-09-16.
  14. "Moise Katumbi Chapwe EMRC" (PDF). EMRC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  15. "Kabila's "Decoupage": an aim at Moise Katumbi's rising popularity". Zambia Reports. 10 Juni 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. "Moïse Katumbi: l'homme, son parcours et ses oeuvres". La conscience. 4 Februari 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-11-10. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. "Necotrans fait l'acquisition d'une importante société de Moïse Katumbi". Jeune Afrique. 9 Novemba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. "RDC: Necotrans rachète Mining Company Katanga de Moïse Katumbi". Radio Okapi. 10 Novemba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  19. "TP Mazembe president". www.tpmazembe.com. Iliwekwa mnamo 2015-09-16.
  20. "2009 CAF Champions League". {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  21. "2010 CAF Champions League". {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  22. 22.0 22.1 "Moise Katumbi - The Abramovich of African football". Ghana Web. 14 Novemba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  23. FIFA.com. "FIFA Club World Cup UAE 2010 - Awards - FIFA.com". FIFA.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-04. Iliwekwa mnamo 2015-09-16. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  24. "FIFA Club World Cup Japan 2015 - TP Mazembe Mazembe - FIFA.com". FIFA.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-20. Iliwekwa mnamo 2015-12-23. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  25. "Katumbi: The Moses of Katanga". African Business Magazine. 4 Aprili 2013.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  26. FIFA.com. "FIFA Committees - Strategic Committee - FIFA.com". FIFA.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-18. Iliwekwa mnamo 2015-09-16. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  27. "The management of Moïse Katumbi attracts CAF". TP Mazembe. 17 Mei 2013.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  28. "- Www.LiveCongo.Com - Tout le Congo en Live !!! -". www.livecongo.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-19. Iliwekwa mnamo 2015-09-16.
  29. 29.0 29.1 "Powerful governor of Congo's copper-rich Katanga province resigns". News Yahoo. 30 Septemba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  30. "Congo's Kabila should receive immunity, says main opponent Katumbi". Reuters. 11 Novemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-03. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  31. "Katumbi wants immunity for Kabila after leaving office". Post Zambia. 13 Novemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-17. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  32. "DRC: Kabila should not face prosecution says main rival Katumbi". UK News Yahoo. 12 Novemba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  33. 33.0 33.1 "Moïse Katumbi: New African Leadership". The Huffington Post. Iliwekwa mnamo 2015-09-16.
  34. "Katanga : l'effet Moïse Katumbi - JeuneAfrique.com". Iliwekwa mnamo 2015-09-16.
  35. "Soccer-Loving Congolese Businessman Eyes Run for Presidency". Bloomberg. 11 Novemba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  36. "Katumbi quits DRC ruling Party". Zambia Reports. 29 Septemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  37. "Millionaire governor gears up for 2016 Congo election bid". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-10. Iliwekwa mnamo 2015-09-16. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  38. Manson, Katrina. "Congo: ‘Katumbi will decide the election’", 20 January 2015. 
  39. "Congolese opposition mulls Katumbi as presidential candidate". Bloomberg. 12 Oktoba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  40. "Powerful governor of Congo's copper-rich Katanga province resigns". Reuters. 29 Septemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2015-10-01.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  41. "Congo's Katumbi signals bid for presidency by quitting party". Bloomberg. 30 Septemba 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  42. Wilson, Tom. "Congo Opposition Parties Demand Election Calendar Be Revised". Bloomberg.com. Iliwekwa mnamo 2015-12-23.
  43. "Moïse Katumbi le gouverneur du Katanga auréolé du prix de bonne gouvernance "Black star of Africa 2012"". Digital Congo. 26 Desemba 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-06-30. Iliwekwa mnamo 2016-02-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  44. "Toure makes it four in a row". CAF. 8 Januari 2015.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)