Mogadishu (kwa Kisomali Muqdisho; kwa Kiitalia Mogadiscio) ni mji mkuu wa Somalia. Iko ufukoni wa Bahari Hindi ikiwa na wakazi milioni 2.590 (2017).

Jiji la Mogadishu
Jiji la Mogadishu is located in Somalia
Jiji la Mogadishu
Jiji la Mogadishu

Mahali pa mji wa Mogadishu katika Somalia

Majiranukta: 2°2′34″N 45°20′18″E / 2.04278°N 45.33833°E / 2.04278; 45.33833
Nchi Somalia
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 2 590 000
Barabara ya Mogadishu inayotenganisha sehemu za kaskazini na kusini za mji pamoja na maeneo ya vikosi tofauti ya wanamgambo (1993).
Helikopta ya Marekani juu ya bandari ya Mogadishu 1993.

Historia

Mogadishu imeundwa mnamo mwaka 900 BK ikawa mji wa kaskazini kabisa wa utamaduni wa Waswahili kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki. Ilikuwa sehemu ya biashara ya kimataifa ya Waswahili jinsi inavyonekana kutokana na sarafu za kale za Uchina, Sri Lanka na Vietnam zilizokutwa na wanaakiolojia katika ardhi yake.

Msafiri Mwarabu Ibn Battuta alitembelea Mogadishu mnamo mwaka 1300 akaona matajiri akataja "watu wanene wengi".

Mji ulikuwa na vipindi vya kujitegemea na vipindi vya kutawaliwa na nchi za nje katika historia yake. Mnamo mwaka 1500 Wareno walikuwa mabwana wake. Tangu katikati ya karne ya 19 Mogadishu ilikuwa chini ya sultani wa Zanzibar.

Mwaka 1892 sultani alikodisha mji kwa Italia iliyoinunua kutoka kwake mwaka 1905 ukawa mji mkuu wa koloni la Somalia ya Kiitalia.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mji ulivamiwa na Waingereza mwaka 1941 waliourudisha kwa Italia mwaka 1954.

Tangu uhuru (1960) Mogadishu ikawa mji mkuu wa Somalia.

Mwaka 1990 dikteta Siad Barre alipinduliwa halafu Mogadishu pamoja na nchi yote iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wanajeshi wa Marekani walijaribu mwaka 1993 kurudisha hali ya usalama kwa niaba ya Umoja wa Mataifa lakini walikuta upinzani mkali kutoka kwa vikundi vya wanamgambo Wasomalia. Baada ya kupoteza askari Marekani iliondoka tena.

Hali ya vita imeendelea hadi mwaka 2012, na kwa muda mrefu nchi ikiwa haina serikali wala bunge na uharamia ulishamiri.

Tazama pia

  Makala hii kuhusu maeneo ya Somalia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mogadishu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.