Moshi (mji)

(Elekezwa kutoka Moshi Mjini)

Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.

Jiji la Moshi

Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Tanzania" does not exist.Mahali pa mji wa Moshi katika Tanzania

Majiranukta: 3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34°S 37.34°E / -3.34; 37.34
Nchi Tanzania
Mkoa Kilimanjaro
Wilaya Moshi Mjini
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi mjini
Msikiti Mkuu wa Moshi

WakaziEdit

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, mji huu una wakazi wapatao 184,292 [1]. Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na Wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kama Wasambaa, Warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.

Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanaenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.

Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.

Hali ya HewaEdit

Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na kipindi cha joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.

UtaliiEdit

Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.

ElimuEdit

Mji wa Moshi una vyuo vikuu vitatu:

  • MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro
  • MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
  • KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini
  • O.U.T(The Open University of Tanzania) ambacho ni tawi la chuo chenye jina hilohilo chenye makao yake makuu jijini Dar es salaam.--

UtawalaEdit

Kiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau na Kilimanjaro.

Mandhari ya Moshi Mjini

MarejeoEdit

  1. Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Moshi MC[dead link]
  Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania  

Boma Mbuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiboriloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Moshi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.