Moyo mkuu

Moyo mkuu ni adili linaloonyesha ukuu wa mitazamo na miguso ya mtu.

Alexander Mkuu akimtendea kwa moyo mkuu mateka wake Mfalme Porus.

Linaendana na utayari wa kukabili magumu na hatari kwa lengo fulani muhimu.

Kwa Kigiriki linaitwa megalopsuchia, ambalo Aristotle alilitaja kama "taji la maadili yote". Kwa Kilatini linaitwa magnanimitas, neno lenye maana ile ya moyo mkuu.