Bofya hapa kuona picha vizuri zaidi

Interwiki ni orodha ya viungo vya mada fulani na makala za kufanana katika wikipedia za lugha nyingine. Inatakiwa kuwepo kila inapowezekana.

Katika ukurasa unaosoma sasa hivi orodha ipo upande wa kushoto nje ya makala chini ya "Lugha zingine". Hapa utaona Deutsch, English, فارسی , Français na kadhalika. Zote ni rangi ya buluu maana ni viungo kwenda kurasa za "Mwongozo wa wikipedia" (Help:Interlanguage links) kwa lugha hizi.

Ukianzisha makala mpya na kuihifadhi utaona bado hakuna majina ya lugha kwa rangi ya buluu.

  • Angalia kwenye dirisha la PC chini kabisa upande wa kushoto.
  • Utaona "Lugha" na chini yake "Add links".
  • Bofya "Add links"
  • Utaona sanduku "Link with page".
  • Ingiza hapa "enwiki" (kwa kawaida, unaweza kuteua pia lugha nyingine..), thibitisha
  • Kwenye sehemu ya "page" andika jina la makala ya Kiingereza (au la makala uliyotafsiri), thibitisha yote, na tena.

Sasa utaona orodha ya lugha zenye viungo kwenda makala za lugha nyingine. Ni msaada mkubwa kama msomaji anataka kusoma maelezo zaidi kwa Kiingereza na kadhalika. Ni msaada pia kwa wahariri wanaosoma lugha hizo wakitafuta habari za nyongeza.

Kusahihisha Interwiki

Ukikuta kiungo cha Interwiki kisicho sahihi (mtumiaji aliyetangulia alikosa kuteua namba sahihi) unaweza kubofya "Hariri viungo". Sasa unafika katika ukurasa wa Wikidata, angalia sanduku ya "Wikipedia", bofya "edit" halafu alama ya ndoo ya takataka ili kufuta neno la Kiswahili. Sasa bofya "publish" na kufunga Wikidata. Ukiita sasa makala yako utaona haionyeshi interwiki tena (inaweza kuchukua dakika kadhaa hadi mabadiliko yanaonekana). Sasa unaweza kuanza upya kuweka interwiki sahihi.

Hatua hizo utatekeleza katika mtazamo wa dawati (Desktop view) inayopatikana kwa kubofya maandishi madogo "dawati" kwenye dirisha la simu yako, chini kabisa.


Jaribu ulichojifunza katika Sanduku la Mchanga