Mstari mnyoofu
(Elekezwa kutoka Mstari ulionyooka)
Mstari mnyoofu (pia: Mstari ulionyooka) ni fikra ya kijiometria. Katika ubapa mstari mnyoofu ni njia fupi kati ya nukta mbili inayoendelea kila upande bila badiliko la mwelekeo. Hauna mwisho au mwanzo wala upana au unene.
Kwa lugha nyingine ni jumla ya nukta zote zilizopo kwenye njia hiyo.
Tena kwa lugha nyingine ni mwelekeo wa nukta inayoelekea mahali bila kubadilisha mwelekeo huu.