Mtakatifu Mauro, O.S.B. (Roma, Italia, 512 - Glanfeuil, Ufaransa, 584) alikuwa mfuasi mpenzi wa Benedikto wa Nursia, kama inavyoelezwa na Gregori Mkuu katika masimulizi manne juu yake ambayo yalitumika sana baadaye katika malezi ya Wabenedikto[1].

"Mt. Benedikto akimuagiza Mt. Mauro kwenda kumuokoa Mt. Plasido", mchoro wa Filippo Lippi, O.Carm. (1445 hivi).

Humo tunasikia kwamba wazazi wake walikuwa wa koo bora za Roma wakamtoa bado mtoto monasterini ili afuate maisha ya kitawa.

Baadaye alijitokeza kwa utiifu wake kwa abati wake na hata kwa miujiza mbalimbali.

Mauro alikuwa mwandamizi wa kwanza wa Benedikto kama abati wa Subiaco[2].

Habari nyingi zaidi zilitungwa katika karne ya 9 lakini si za kuaminika.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu tarehe 15 Januari, au, pamoja na mwenzake Plasido, tarehe 5 Oktoba.[3]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Vyanzo hariri

  • Gardner, Edmund G. (editor) (1911. Reprinted 2010). The Dialogues of Saint Gregory the Great. Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 978-1-889758-94-7. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-06-07. Iliwekwa mnamo 2016-12-10.  Check date values in: |date= (help)
  • Rosa Giorgi; Stefano Zuffi (ed.), Saints in Art (Los Angeles: Getty Publications, 2003), 272.
  • John B. Wickstrom: "Text and Image in the Making of a Holy Man: An Illustrated Life of Saint Maurus of Glanfeuil (MS Vat. Lat. 1202)," Studies in Iconography 14(1994), 53-85.
  • Ibid. The Life and Miracles of St. Maurus: Disciple of Benedict, Apostle to France (Kalamazoo, Cistercian Publications, 2008).

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.