Kesi ya Joseph Spell, Jimbo la Connecticut v. Joseph Spell, Ilikuwa kesi ya kisheria ya mwaka 1940 ambapo mshtakiwa mmarekani mwenye asili ya Kiafrika kwa jina Joseph Spell alishtakiwa kwa kumbaka Eleanor Strubing, mwanamke tajiri mzungu ambaye alikuwa bosi wake.[1] Mashtaka na kesi hiyo ilipamba kwenye vichwa vya habari vya kustaajabisha. Spell aliwakilishwa na Samuel Friedman na jaji wa baadaye wa Mahakama ya Juu ya Marekani anayeitwa Thurgood Marshall. Kesi hiyo imeangaziwa katika filamu ya Marshall ya mwaka 2017.[2]

Spell, aliyekua mmarekani mwenye asili ya Kiafrika (mmarekani mweusi), [3] alifanya kazi kama dereva binafsi kwa mwanamke tajiri mzungu aitwaye Eleanor Strubing. Baada ya kuhojiwa kwa saa 17, Spell alikiri kuwa na uhusiano wa karibu naye, lakini (kinyume na maelezo ya polisi) alisema kwamba hajawahi kukiri kumbaka. Jopo la majaji mwaka 1940 lilimuondoa katika hatia ya kutokuwa na hatia ya ubakaji.

Historia ya Nyuma

hariri

Spell alizaliwa Lafayette, Louisiana mwaka 1909.Alihudumu kwa miaka sita katika Jeshi la Marekani kabla ya kuondolewa kwa sababu ya ulevi, kuiba gari la afisa, na kuligonga. Alifunga ndoa akiwa na umri wa miaka 17, alitengana na mkewe baada ya miezi mitatu, lakini hakupata talaka, na alikuwa akiishi katika attic (chumba cha chini ya nyumba) ya nyumba ya mwajiri wake na mwenzi wake Virgis Clark, ambaye aliajiriwa na Strubings kama mpishi.[3][4]

Marejeo

hariri
  1. TIMES, Special to THE NEW YORK (1940-12-12), "Mrs. J.K. Strubing Is Kidnapped And Hurled Off Bridge by Butler; WOMAN KIDNAPPED; HURLED OFF BRIDGE", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2022-12-13
  2. https://apnews.com/07057e2c78f2451193e55df5968aa53c
  3. 3.0 3.1 "Legal Affairs". www.legalaffairs.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-04. Iliwekwa mnamo 2022-12-13. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. Smithsonian Magazine, Lorraine Boissoneault. "The True Story Behind "Marshall"". Smithsonian Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kesi ya Joseph Spell kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.