Hajj Maulid Makokha ni Mkenya kutoka eneo la magharibi mwa nchi. Alizaliwa katika mji wa Mumias katika miaka ya themanini na kukulia huko. Babu yake aliitwa Hamisi Masimba aliyekuwa mwanajeshi wa majini, naye baba yake ni Roman na mama yake ni Alice, aliyetoka katika familia ya heshima ya Wilson Okusimba, aliyekuwa chifu wa heshima mno katika zama za ukoloni.

Alisomea elimu ya msingi katika shule kadhaa kama vile shule ya msingi ya wavulana ya St. Peter's Mumias, kisha akahamia shule ya msingi ya Mwitoti na hatimaye shule ya msingi ya Kaloleni Muslim iliyoko Kisumu, ambapo alipata cheti cha KCPE mnamo mwaka wa 2002.

Maulid alisoma masomo yake yote ya shule ya upili katika shule ya upili ya Abrar huko Eldoret na kupata cheti cha KCSE kama mwanafunzi bora zaidi kuwahi kutoa alama ya A- katika shule hiyo mwaka wa 2006.

Mnamo mwaka wa 2008, alisafiri hadi Sudan kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu, ambapo baada ya kumaliza masomo ya lazima ya lugha ya Kiarabu katika muda wa mwaka mmoja, alisafiri hadi Saudi Arabia kwa ajili ya masomo ya Sheria ya Kiislamu (Shari'ah) katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Madina, ambapo alihitimu mwaka wa 2012 kwa heshima ya daraja la kwanza. Baadaye alijiunga na programu ya uzamili katika elimu ya Kiislamu na kuhitimu shahada ya uzamili mwaka wa 2019.

Alifanya kazi katika nyadhifa kadhaa kama mwalimu, mshauri na meneja msaidizi; kuanzia fani ya elimu, ambapo alifundisha masomo ya Kiarabu na Kiislamu katika shule za msingi na sekondari jijini Nairobi. Baadaye alijiunga na sekta ya benki ya Kiislamu hadi sasa.

Familia

hariri

Maulid Makokha ana mtoto mvulana mmoja na wasichana wanne: Leila, Sidra, Mohammed, Fatuma na Shukri.