Majimbo ya Sudan Kusini ni vitengo vya Jamhuri ya Sudan Kusini yenye madaraka ya kujitawala kulingana na katiba ya nchi. Kila jimbo huwa na bunge na serikali yake inayoongozwa na gavana.

Migawanyiko ya kiutawala ya Sudan Kusini imejumuishwa katika majimbo matatu ya kihistoria ya:storical provinces of:      Bahr el Ghazal      Equatoria      Greater Upper Nile

Idadi ya majimbo ni 10. Majimbo hayo yaliundwa kutoka kwa majimbo matatu ya kihistoria ya zamani (ambayo ni pia kanda za kisasa) ya Bahr el Ghazal (kaskazini-magharibi), Equatoria (kusini), na Greater Upper Nile (kaskazini mashariki). Majimbo hayo yamegawanywa zaidi katika wilaya (counties) 79 .

Mnamo Oktoba 2015, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit alitangaza kugawa majimbo hayo 10 kuwa 28. Mwezi Novemba 2015 bunge la Sudan Kusini liliidhinisha kuundwa kwa majimbo mapya. Mnamo Januari 2017, Rais Salva Kiir alitangaza amri ya kuongeza tena idadi ya majimbo kutoka 28 hadi majimbo 32. [1]

Lakini kwenye Februari 2020 nchi ilirejea katika majimbo 10 ya awali pamoja na maeneo mawili ya kiutawala, Pibor na Ruweng, na eneo la hali maalum ya kiutawala la Abyei . [2] [3] Mabadiliko hayo yalikuwa tokeo la makubaliano ya amani yaliyomaliza Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Sudan Kusini,

Eneo la Abyei linachukuliwa kuwa sehemu ya Jamhuri ya Sudan na Jamhuri ya Sudan Kusini kwa wakati mmoja. Eneo la Kafia Kingi linazaniwa kati ya Sudan Kusini na Sudan na Pembetatu ya Ilemi inazaniwa kati ya Sudan Kusini na Kenya.

Majimbo kumi na maeneo matatu (2020-sasa)

Bendera Dola au eneo Makao makuu Gavana au

Afisa mkuu

Wakazi
(2010)[4]
Eneo
(km2)[4]
Densiti
(/km2)
Kanda
  Bahr el Ghazal Kaskazini Aweil Tong Aken Ngor 820,834 30,543.30 26.87 Bahr el Ghazal
  Bahr el Ghazal Magharibi Wau Sarah Cleto Rial 358,692 91,075.95 3.94 Bahr el Ghazal
  Lakes Rumbek Rin Tueny Mabor 782,504 43,595.08 17.95 Bahr el Ghazal
  Warrap Kuajok Aleu Ayieny Aleu[5] 1,044,217 45,567.24 22.92 Bahr el Ghazal
  Western Equatoria Yambio Alfred Futiyu 658,863 79,342.66 8.30 Equatoria
  Central Equatoria Juba Emmanuel Adil Anthony 1,193,130 43,033.00 27.73 Equatoria
  Eastern Equatoria Torit Louis Lobong Lojore 962,719 73,472.01 13.10 Equatoria
  Jonglei Bor Denay Jock Chagor 1,228,824 80,926.00 TBD Greater Upper Nile
  Unity Bentiu Joseph Monytuil 399,105 TBD TBD Greater Upper Nile
  Upper Nile Malakal Budhok Ayang Kur[6] 1,013,629 77,283.42 13.12 Greater Upper Nile
  Eneo la Abyei Abyei Kuol Deim Kuol 124,390 10,546.00 TBD Bahr el Ghazal
  Eneo la Pibor Pibor Lokali Amae Bullen[7] 214,676 41,962.00 TBD Greater Upper Nile
  Eneo la Ruweng Pariang Stefano Wieu Mialek[8] 246,360 TBD TBD Greater Upper Nile

Marejeo

  1. "South Sudanese President creates four more states – Sudan Tribune: Plural news and views on Sudan". www.sudantribune.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-18. Iliwekwa mnamo 1 March 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "South Sudan Kiir agrees to re-establish the 10 states - Sudan Tribune: Plural news and views on Sudan". www.sudantribune.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-01. Iliwekwa mnamo 15 February 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Kiir agrees to relinquish controversial 32 states". Radio Tamazuj (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 15 February 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. 4.0 4.1 "Statistical Yearbook for Southern Sudan 2010". Southern Sudan Centre for Census, Statistics and Evaluation. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 October 2012. Iliwekwa mnamo 1 June 2012.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  5. "Kiir fires Warrap governor, appoints a successor". Radio Tamazuj (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-24. 
  6. "Budhok Ayang Kur appointed Governor of Upper Nile state". South Sudan FP (kwa Kiingereza). 29 January 2021. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-12-08. Iliwekwa mnamo 2 February 2021.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. "New Pibor chief administrator vows to restore peace, security". Radio Tamazuj (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-24. 
  8. "South Sudan's Kiir sacks Ruweng chief administrator". June 6, 2022. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-09. Iliwekwa mnamo 2023-03-19.  Check date values in: |date= (help)