Mtumiaji:Shikolyo Muzamil/Naphazoline
Naphazoline, inayouzwa chini ya majina mengi ya chapa, ni dawa inayotumika kutibu pua iliyoziba au uwekundu wa macho kutokana na kuwashwa kidogo.[1] Dawa hii inapatikana kama dawa ya pua au matone ya macho.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutoona vizuri na kuumwa umwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kujirudia kwa kuziba kwa pua baada ya kuacha kuitumia, maumivu ya kichwa, mapigo ya moyo na woga.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii hufanya kazi kwa kuamilisha kipokezi cha alpha adrenergic ambacho hufanya mishipa midogo kuwa myembamba.[1]
Naphazoline ilipewa hati miliki mwaka wa 1934 na ikaanza kutumika katika matibabu mwaka wa 1942.[2] Dawa hii inapatikana kama dawa ya kawaida na kwenye kaunta.[1] Nchini Marekani mililita 15 za kioevu chake hugharimu dola 14 takriban za Marekani.[3]
References
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Naphazoline Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "AHFS2021" defined multiple times with different content - ↑ Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 552. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-29. Iliwekwa mnamo 2020-10-19.
- ↑ "Naphazoline ophthalmic Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
[[Category:Madawa]]