Misuli [1] ni sehemu ya mwili wa wanyama na binadamu inayowezesha mwendo wa viungo vyake. misuli inaundwa na tishu ya pekee yenye uwezo wa kujinywea na kulegea. Wakati wa kujinywea huwa mifupi zaidi. Kwa njia hii misuli inayounganishwa na mifupa ya mkono au mguu huleta mwendo wa viungo hivi.

Kazi ya musuli mkononi.
Aina za musuli:
misulia milia, misuli myororo, misuli ya moyo

Aina za musuli

hariri

Misuli hutofautishwa kwa namna mbalimbali:

  • kama ni misuli ridhia inayoendeshwa kwa hiari maana tunaamua kuzinywea au kuzilegeza (kama misuli ya kusogeza mkono) au misuli sihuria inayoendeshwa bila hiari (kama misuli inayoendesha mwendo wa utumbo)
  • kufuatana na umbo na muundo wa misuli kama ni misuli milia (striped muscle) au misuli myororo (smooth muscle)

Mara nyingi hutofautishwa namna tatu za misuli:

  • misuli kiunzi iinayounganishwa na mifupa kwa ukano. Hii misuli inasababisha mwendo wa mifupa ya viungo na kuendeshwa kwa ridhia ya mtu kwa hiyo inaitwa pia misuli ridhia. Katika mwili wa mwanaume wastani hii misuli kiunzi ni takriban asilimia 42 ya masi ya mwili wake; kwa mwili wa mwanamke wa wastani hii misuli ni 36 % ya masi ya mwili. Hiyo ndiyo sababu ya kwamba kwa wastani wanaume wana nguvu kuliko wanawake.
  • misuli msisima ambayo haiunganishwi na mifupa na kuendesha mwendo wa viungo vya ndani vya mwili kama utumbo, mapafu, mizizi ya nywele au mishipa ya damu. Misuli hii hiongozwi kwa ridhia huitwa misuli sihuria.
  • misuli ya moyo ni misuli sihuria lakini kwa umbo hufanana zaidi na misuli kiunzi. Wakati misuli hii inajikaza inasukuma damu kwenda mishipa ya damu upande moja na ikilegea upande mwingine kupokea damu kutoka mishipa.

Misuli milia

hariri

Misuli ya kiunzi na moyo huitwa pia "misuli milia" kutokana na milia inayoonekana usoni mwao. Milia hii inatokana na muundo wa misuli hii inayofanywa na vinyuzi virefu vya rangi mbili vinavyopangwa taratibu katika misuli na kuonyesha milia meupe na mekundu kwa kubadilishana. Vinyuzi vyekundu ni protini za kiaktini na vinyuzi vyeupe ni protini kimiosi.

Muundo wa misuli

hariri

Misuli inaundwa na seli za pekee zenye uwezo wa unyweo. inatekeleza unyweo baada ya kupokea kiamshi kupitia neva. Kiamshi ni mshtuko wa umeme unaopitishwa kutoka seli kwenda seli nyingine. Seli za misuli huwa na protini za kiaktini na kimiosini.

Unyweo wa misuli

hariri

Wakati misuli inapokea kiamshi kutoka neva nafasi katika utando wake inapitisha kalsi na kalsi inasababisha aina mbili za protini kuingiliana hivyo kufupisha urefu wa misuli.

Jinsi ya kuunda misuli

hariri
  • Anza polepole. Kuunda misuli huchukua muda mrefu na haifai ujiweke presha kupata misuli kwa muda mfupi.
  • Kuwa na mpango na mikakati unayofuata ili kuweza kuifikia kama vile mipango ya wakati wa kufanya mazoezi, kuinua chuma au kula.
  • Chakula kina maana sana katika misuli haswa protini ambayo wafaa uile kwa wingi. Maji pia ni muhimu kwa umetaboli.
  • Fuata mikakati uliyopanga na usife moyo hata usipoona matokeo kwa haraka.

Marejeo

hariri
  1. "Misuli latokana na Kilatini/Kiingereza "musculus"/"muscle". Neno la Kilatini lamaanisha "panya mdogo" kwa sababu wazee walilinganisha umbo la misuli ya kujinywea na umbo la panya mdogo anayejificha chini ya ngozi.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Musuli kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.