Muziki wa kielektroniki

Muziki wa kielektroniki (au Muziki elektroniki) ni aina ya muziki unaotolewa kwa njia ya vifaa vya elektroniki na vipaza sauti.

RCA Mark II synthesizer.

Kimsingi kuna aina mbili ya muziki huo:

  • muziki unaotolewa kwa ala za muziki zinazotoa mitetemo halisi zinazopokewa kwa njia ya elektroniki, kubadilishwa na kusikiwa kupitia kipaza sauti, kwa mfano gitaa ya umeme
  • kompyuta au vifaa kama synthesizer na kinanda cha kielektroniki vinavyotoa mishtuko ya umeme inayotolewa kama sauti kwa njia ya kipaza sauti.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia wanamuziki mbalimbali walianza kufanya majaribio ya kutoa muziki kwa njia ya vifaa vya umeme. Tangu miaka ya 1980 bendi kadhaa zilianza kutumia mbinu hizo na kufaulu.

Kwa jumla matumizi ya sauti za elektroniki yamepanua sana namna za muziki zinazoweza kutolewa.

Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muziki wa kielektroniki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.