Mwali
Mwali (au Moheli) inayoitwa pia ni moja kati ya visiwa vitatu vinavyounda nchi ya kisiwani ya Komori katika Bahari Hindi. Mwali ni kisiwa kidogo kati ya visiwa vikuu vya Komori.
Idadi ya wakazi wake ni mnamo watu 38,000 (mwaka 2006). Mji mkuu ni Fomboni. Wakazi wake ni mchanganyiko wa watu wenye asili ya Wabantu, Waarabu, Wamalay na Wamadagaska.
Dini ya wakazi wengi ni Uislamu wa Kisunni.
1997 Mwali ilijitenga na nchi ya Komori lakini ilirudi mwaka 1998.