Mwamvita Makamba
Mwamvita Makamba ni mwanamke Mtanzania mwenye ujuzi katika sekta ya mawasiliano ya simu katika masoko na kuwa na ufahamu wa karibu unaohitajika kuendesha kampuni katika ustawi na pia kudumisha uwajibikaji wake kwa jamii.
Mwamvita Makamba | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Kazi yake | mwanaharakati |
Elimu yake
haririMwamvita alisoma shule nyingi mahali tofauti nchini Tanzania kwani baba yake alikuwa mtumishi wa umma, hivyo ilimpasa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mara kwa mara. Katika elimu yake ya msingi alisoma Handeni, Lushoto na Morogoro. Alipohitimu elimu yake ya msingi alijiunga na shule ya sekondari ya wasichana Kifungilo girls kwa kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.
Baadae alijiunga na shule ya sekondari ya wasichana Kilakala mkoani Morogoro. Katika shule ya Kilakala alisoma kwa muda mfupi mpaka alipokuja kujiunga na shule ya sekondari Shaaban Robert huko jijini Dar es Salaam mpaka alipohitimu elimu ya sekondari. Alipokuwa kwenye shule ya Shaaban Robert. Mwamvita na wenzake waliweza kuanzisha shirika lililojulikana kwa jina la OYA, shirika hili lilikua kama jukwaa la vijana kwa ajili ya kupaza sauti za vijana.
Baadae aliweza kujiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo alisomea shahada ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma na baadae masters katika Siasa na Mahusiano ya Kimataifa. [1]
Kazi yake
haririMwamvita alianza kuwa mwanaharakati kuanzia alipokua mwanafunzi shule ya sekondari ambapo pamoja na wenzake aliweza kuanzisha shirika lililoitwa OYA, shirika hili lilikua ni jukwaa la vijana kupaza sauti katika mambo kadha wa kadha yanayowagusa vijana.
Alipokua Chuo Kikuu alikua anafanya kazi katika shirika la TCD(Tanzania Center for Democracy) ambapo alikua akijihusisha na vijana wa vyama vyote vya siasa ili kuweza kutetea ukombozi wa kijamii wa vijana. Hivyo alikua sauti ya vijana. Aliweza kujihusisha katika siasa na kazi ya Wingamizi wa Chama Cha Mapinduzi, UVCCM.
Baada ya hapo mwaka 2008, Mwamvita alijiunga na kampuni ya Vodacom. Hii ndiyo ilikua kazi yake ya kwanza kabisa rasmi ya kuajiriwa. [2] Mwamvita amechukua nafasi nyingi katika kiwango cha Exco ndani ya Vodacom Tanzania, pamoja na kua kiongozi wa Mambo ya Biashara na Masoko, kabla ya kujiunga na Vodacom International ambako alifanya kazi kama Mshirika wa Utendaji wa Biashara kwa Mambo ya Shirikisho ya kusimamia Agenda za Uwekezaji wa Jamii. Pia alishiriki jukumu la kusaidia mkakati wa upanuzi wa Vodacom katika masoko mapya katika Afrika Kusini mwa Sahara.
Hivi sasa, Mwamvita ni mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Biashara ya Pan Africa kwa Vodacom Business Africa na Unit Enterprise. Pia ni mwanabodi katika Bodi ya Wadhamini wa Vodafone Group Foundation ambapo amewakilisha biashara za masoko ya Vodafone kwa miaka mitano iliyopita. Kwa uwezo huu, Mwamvita anasimama na kutekeleza mipango muhimu ya Uwekezaji wa Jamii ya Jamii kama vile mradi wa kuondokana na Fistula nchini Tanzania ambao una dhima ya kukomesha Fistula Tanzania mwaka 2016.
Tuzo zake
haririKimataifa, Mwamvita ametambulika na Idara ya Jimbo la Marekani kama 'Mwanamke wa Nguvu ', ambapo kutambulika huku kumempa nafasi ya kushirikiana uzoefu wake na Wanawake wengi wenye nguvu zaidi ya 500 nchini Marekani huku wakiendeleza ujuzi wake wa uongozi.
Mwamvita Makamba alipewa tuzo ya wanawake wa Tanzania ya tuzo ya mafanikio mwaka 2011.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwamvita Makamba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |