Mwanaanthropolojia

Mwanaanthropolojia ni mtu anayejihusisha na taaluma ya anthropolojia, yaani uchunguzi wa mambo yanayohusiana na binadamu katika jamii za zamani na za sasa.[1][2][3]

Kuna aina mbalimbali za anthropolojia, kama vile anthropolojia ya kijamii, anthropolojia ya kitamaduni na anthropolojia ya kifalsafa ambazo huchunguza kanuni, maadili, na tabia za jumla za jamii.

Anthropolojia ya lugha huchunguza jinsi lugha inavyoathiri maisha ya kijamii, wakati anthropolojia ya kiuchumi inachunguza tabia za kiuchumi za binadamu. Anthropolojia ya kibiolojia, anthropolojia ya kimahakama na anthropolojia ya kitabibu huchunguza maendeleo ya kibiolojia ya binadamu, matumizi ya anthropolojia ya kibiolojia katika mazingira ya kisheria, na uchunguzi wa magonjwa na athari zake kwa binadamu kwa kipindi kirefu, mtawalia.

Marejeo

hariri
  1. "anthropology". Oxford Dictionaries. Oxford University Press. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Oktoba 2, 2013. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "anthropology". Encyclopædia Britannica. https://www.britannica.com/EBchecked/topic/27505/anthropology.
  3. "What is Anthropology?". American Anthropological Association. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)