Mwaura Isaac Maigua

Isaac Maigua Mwaura (amezaliwa Mei 29, 1982) kwa sasa ndiye Msemaji wa Serikali ya Kenya, kabla ya nafasi hiyo amewahi kuhudumu katika nafasi ya Seneta, Katibu Tawala wa Baraza la Mawaziri (CAS) - Naibu Waziri katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri.

Mwaura aliwahi kuwa Seneta katika Seneti ya Kenya kwa tiketi ya Chama cha Jubilee kati ya 2017 na 2022 ambapo aliteuliwa kuwakilisha Watu Wenye Ulemavu katika kipindi hicho. Alikuwa mtu wa tatu kushika nafasi hiyo chini ya Katiba ya Kenya ya mwaka 2010, Pia alihudumu kwa nafasi ya ubunge katika Bunge la Kitaifa kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 baada ya kuteuliwa na Chama cha Orange Democratic Movement kuwakilisha Makundi maalum.

Historia

hariri

Mwaura alikuwa Mbunge wa kwanza wa Bunge la Kitaifa na Seneta nchini Kenya mwenye ualbino. Yeye ni mwanachama wa United Democratic Alliance Party (UDA) ambacho ni chama tawala chini ya Utawala wa Kenya Kwanza wa Rais William Samoei Ruto.

Marejeo

hariri