Mwerezi ni mti wenye historia katika nchi ya Lebanon.

Historia ya mwerezi wa Lebanon inaanzia miaka mingi nyuma kabla Yesu [[hajazaliwa, kwa mfano katika Zaburi 92:12, "Wenye haki watastawi kama mtende]], watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni".

Ni mti unaostahimili hali za baridi kali na joto pia.

Mwerezi hukua taratibu sana na hivyo kuufanya kuwa mti wenye mbao imara. Kwa sababu hiyo mierezi ya Lebanon imekuwa ikikatwa kwa wingi tangu enzi za mfalme Suleiman (na wafalme wengine pia) ambaye aliitumia mierezi ya Lebanon katika ujenzi wa hekalu la Yerusalemu.

Mierezi ya Lebanon imekuwa pia ikitumiwa na wenyeji wake kutengenezea mashua ambazo ziliwawezesha kuwa wafanyabiashara wa kwanza wa kimataifa.

Kutokana na ukataji uliokithiri, mierezi imekuwa michache sana katika nyakati hizi. Kwa mfano kusini mwa Lebanon ni ngumu hata kuamini kwamba kuliwahi kuwa na misitu yenye miti mikubwa na kuiletea sifa nchi ya Lebanon. Imebaki miti michache katika maeneo ya kaskazini karibu na mpaka wa Syria.

Kutokana na historia iliyotukuka ya mwerezi, mti huo umewekwa katikati ya bendera ya nchi ya Lebanon na kuwa miongoni mwa alama muhimu za taifa la Lebanon.