Open main menu

Uingereza

nchi ya visiwa katika Ulaya Kaskazini-Magharibi, sehemu ya Ufalme wa Muungano
(Elekezwa kutoka Mwingereza)
England
Uingereza
English Flag English Coat of Arms
(Bendera ya Uingereza) (Nembo la Uingereza)
Wito (Kifaransa): Dieu et mon droit
("Mungu na haki yangu")
Uingereza katika Ulaya
Uingereza kwenye visiwa vya Britania
Mahali pa Uingereza (kijani cheusi) kwenye visiwa vya Britania ndani ya Ufalme wa Muungano (kijani nyeupe) pamoja na Jamhuri ya Eire (buluu) upande wa magharibi
Lugha Kiingereza
Mji Mkuu London
Mji Mkubwa London
Eneo
– jumla

130,395 km²
Wakazi

2004
–sensa ya 2001
– Msongamano wa watu

50.1 millioni [1]

49,138,831 [2]
377/km²

Umoja wa nchi yote 927 BK na mfalme
Athelstan
Dini rasmi Church of England (Anglikana)
Pesa Pound sterling (£) (GBP)
Masaa UTC / (GMT)
Summer: UTC +1 (BST)
Ua la Taifa Waridi ya Tudor (nyekundu, nyeupe)
Mtakatifu wa kitaifa Mt George

Uingereza (pia: Ingilandi, England) ni nchi kubwa ndani ya Ufalme wa Muungano yenye wakazi milioni 50 au 83% ya wakazi wa Ufalme wote na eneo lake ni theluthi mbili ya kisiwa cha Britania.

Katika lugha ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa chote cha Britania. Lakini hali halisi "Uingereza" ni ile sehemu kubwa zaidi kwenye kisiwa kile pamoja na Uskoti (Scotland) na Welisi (Wales).

Asili ya jina la Kiswahili ni neno "إنجليزي injilisi (matamshi ya Kimisri: ingilisi)" katika lugha ya Kiarabu na kwa namna ya Kibantu sauti ya "l" ikawa "r"; Waarabu walipokea jina kutoka kwa Kihispania "Ingles" ambalo ni neno lao kwa Mwingereza.

Yaliyomo

JiografiaEdit

Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambayo ni kisiwa kikubwa cha Ulaya. Imepakana na Welisi upande wa magharibi na Uskoti upande wa kaskazini. Mji Mkuu ni London. Ufaransa iko upande wa kusini ng'ambo ya Mfereji wa Kiingereza. Tangu mwaka 1994 kuna njia ya reli kwa tobwe chini ya mfereji inayounganisha Uingereza na Ufaransa.

Kati ya miji mikubwa ya Uingereza ni: London, Manchester, Birmingham, Leeds, Sheffield, Bradford na Liverpool.

Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni Isle of Wight katika kusini.

Mito ya UingerezaEdit

 
Mto Thames katika London mnamo mwaka 1750

Mikoa ya UingerezaEdit

Makala kuu: Mikoa ya Uingereza

HistoriaEdit

Uingereza ilikaliwa na makabila ya Wabritania wenye lugha za Kikelti na kuvamiwa na Dola la Roma katika karne ya pili BK. Ikawa sehemu ya Dola la Roma hadi karne ya tano BK. Wakati ule Waroma walipaswa kuondoa wanajeshi wao kisiwani kwa ajili ya ulinzi wa nchi za bara.

Uvamizi wa Waanglia-SaksoniEdit

Katika karne za 5 na 6 BK makabila ya Kigermanik walivamia kisiwa hasa Wasaksoni, Waanglia na Wadenmark. Walileta lugha zao za Kigermanik zilizochukua nafasi ya lugha ya Wabritania.

Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au Cornwall au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda Britania Ndogo (Kiingereza:Brittany; Kifaransa: Bretagne).

Karne zilizofuata kisiwa kiliona madola madogo na hali ya vita. Mwaka 937 Mfalme Athelstan aliweza kuunganisha karibu eneo lote la Uingereza ya leo.

Uvamizi wa WanormaniEdit

Mwaka 1066 wanajeshi Wanormani kutoka kaskazini ya Ufaransa walivamia Uingereza na kuteka yote chini ya mtemi William Mshindi. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha Kiingereza.

Ufalme wa MuunganoEdit

Tangu mwaka 1601 mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na wafalme wa pamoja hadi mwaka 1707. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania. Tangu 1801 jina likawa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland) hadi 1927 wakati sehemu kubwa ya Eire ikapata uhuru wake. Tangu 1927 Uingereza ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).

 
Mji wa Liverpool

MarejeoEdit

  1. Office for National Statistics - UK population approaches 60 million
  2. Office for National Statistics - 2001 census Population profile - England.

Viungo vya njeEdit