NACADA Kenya (kifupisho cha: National Agency for the Campaign against Drug Abuse) ni taasisi ya serikali ya Kenya ambayo inapigana na matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya.

Historia ya NACADA Kenya hariri

Dhana kuhusu NACADA Kenya ilianzishwa mwaka 1996 wakati kamati ya kuangalia utumizi wa dawa vibaya ilianzishwa.

Baadaye, mwaka 2001, NACADA Kenya ilitengenezwa. Minajili yake wakati huo ilikuwa kuwaelimisha hasa vijana kuhusu kujiepusha na matumizi ya mihadarati na jinsi ya kujiepusha na ulevi.

Kazi ya NACADA Kenya hariri

  • Kuelimisha kuhusu kujiepusha na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
  • Kuwafanya watu wawajibike kuhusu dawa.
  • Kuhakikisha kuwa washikadau wote wamewajibika kuhusu dawa .
  • Kuwa nyapara kuona kuwa dawa zinazotengenezwa zinafanya kazi inayostahili.