NALA Money ni application ya kifedha iliyoanzishwa mwaka 2017 ambayo inatoa huduma ya miamala ya kifedha kama vile kufanya malipo na kutuma fedha Afrika nzima[1]

Kampuni ya NALA Money ipo kwenye baadhi ya nchi za Afrika kama vile Tanzania, Kenya na Uganda tena ipo nchini Marekani na Uingereza. Kwa sasa, NALA haitozi gharama yoyote ile kwa mteja afanyapo miamala ila makato yapo kama kawaida kwenye huduma za kibenki au mitandao ya simu.

Pamoja na wepesi wa kufanya miamala,watumiaji wa NALA wanaweza kufahamu taarifa fupi kuhusu historia ya miamala yao iliyofanyika iwe ya kibenki au mitandao ya kifedha[2]

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nala Money kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.