Napoleon III (Charles Louis Napoléon Bonaparte; 20 Aprili 1808 – 9 Januari 1873) alikuwa rais wa kwanza wa Ufaransa (kama Louis-Napoléon Bonaparte) kutoka 1848 hadi 1852 na Kaizari wa Ufaransa kutoka 1852 hadi 1870. Alikuwa mpwa wa Napoleon I na mfalme wa mwisho kutawala Ufaransa.

Taswira ya Napoleon III mnamo 1865

Vyeo hariri

Alichaguliwa kwa urais wa Jamhuri ya Pili ya Kifaransa mnamo 1848, alitwaa madaraka kwa nguvu mnamo 1851, wakati hakuweza kuchaguliwa tena kikatiba; baadaye alijitangaza kuwa Kaizari wa Ufaransa. Alitawala hadi kushindwa katika vita dhidi ya Ujerumani na kutekwa kwake na Prussia na washirika wake kwenye Mapigano ya Sedan mnamo 1870.

Hitimisho hariri

Napoleon III alikuwa mtawala maarufu aliyependwa na sehemu kubwa ya raia wake, ambaye alitumia kura za maoni kuongoza siasa yake. Alisimamia mabadiliko ya uchumi wa Ufaransa.

Aliwekeza sana katika miundombinu za nchi akaagiza kujengwa kwa idadi kubwa ya meli zabiashara na kivita. Alipanua maeneo ya koloni za Ufaransa.

Alishiriki katika Vita ya Italia ya 1859 akaamuru kuanzisha Vita ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani ya 1870 ambapo aliongoza wanajeshi wake wakati wa mapigano na akakamatwa.

Siasa ya ndani na ya kiuchumi hariri

Napoleon III aliagiza ujenzi mpya wa Paris uliotekelezwa na Georges-Eugène Haussmann, akienelea kupanusha mfumo mzuri wa bustani kubwa za starehe kwenye jiji. Alizindua miradi ya kazi za umma kama hiyo katika miji mingine yote mikubwa nchini Ufaransa.

Alipanua na kuimarisha mfumo wa reli kwa taifa lote, na pia akafanya kazi ya kuboresha mfumo wa benki.

Napoleon III aliendeleza ujenzi wa Mfereji wa Suez na kuanzisha kilimo cha kisasa, ambacho kilimaliza njaa nchini Ufaransa na kuifanya nchi kuwa muuzaji nje wa mazao.

Alifanya mapatano na Uingereza kuhusu Mkataba wa Biashara Huria na makubaliano kama hayo na mataifa mengine ya Ulaya.

Katika siasa ya kijamii alikubali kuwapa wafanyakazi wa Ufaransa haki ya kugoma na haki ya kuunda vyama vyao. Wanafunzi wa kwanza wa kike walidahiliwa huko Chuo Kikuu cha Sorbonne na fursa za elimu kwa wanawake ziliongezeka. Chini yake orodha ya masomo yanayotakiwa kufundishwa shuleni ilipanushwa vievie.

Siasa ya Nje hariri

Katika siasa ya nje, Napoleon III alilenga kurudisha athira ya Ufaransa huko Ulaya na ulimwenguni kote.

Katika Ulaya, alijiunga na Uingereza na kuishinda Urusi katika Vita ya Krim (1853-1856). Siasa yake ilisaidia kuungana kwa Italia kwa kushinda Dola la Austria katika Vita ya Italia ya 1859. Baadaye alipata maeneo ya Savoy na Nice kama shukrani kwa msaada wake. Wakati huo huo, vikosi vyake vilitetea Dola la Papa dhidi ya kuunganishwa na Italia.

Alisaidia pia maungano wa mikoa kwenye mto Danubi yaliyoendelea kuwa Temi za Moldavia na Wallachia.

Napoleon III aliongeza koloni za Ufaransa mara mbili kwa upanuzi katika Asia, Pasifiki na Afrika.

Kwa upande mwingine, alishindwa kabisa alipojaribu kuingilia kati ndani ya Meksiko alichotaka kufanya kuwa nchi chini ya ulinzi wa Ufaransa.

Ugomvi na Prussia hariri

Kuanzia 1866, Napoleon III alilazimika kukabili nguvu iliyoongezeka ya Prussia kwani waziri mkuu wake Otto von Bismarck alilenga kujenga umoja wa madola ya Kijerumani chini ya uongozi wa Prussia.

Mnamo Julai 1870, Napoleon III alifuata wito wa wanasiasa na waanchi wengi akatangaza vita dhidi ya Prussia, ingawa alikuwa na wasiwasi.

Bila washirika akiwa na jeshi dhaifu, Ufaransa ilishindwa haraka wakati Napoleon III alikamatwa katika mapigano ya Sedan. Aliondolewa cheo cha kifalme na Jamhuri ya Tatu ya Kifaransa ilitangazwa huko Paris. Alikwenda uhamishoni Uingereza, ambapo alikufa mnamo 1873.

Marejeo hariri

Maandiko ya Napoleon III hariri

  • Des Idées Napoleoniennes – an outline of Napoleon III's opinion of the optimal course for France, written before he became Emperor.
  • History of Julius Caesar – a historical work he wrote during his reign. He drew an analogy between the politics of Julius Caesar and his own, as well as those of his uncle.
  • Napoleon III wrote a number of articles on military matters (artillery), scientific issues (electromagnetism, pros and cons of beet versus cane sugar), historical topics (the Stuart kings of Scotland), and on the feasibility of the Nicaragua canal. His pamphlet The Extinction of Pauperism (OCLC 318651712, Kigezo:JSTOR) helped his political advancement.

Kujisomea hariri

Wasifu hariri

Vyanzo vya sekondari hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: