Natalie Grant (amezaliwa tar. 21 Desemba 1971, mjini Seattle, Washington) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za kisasa za Kikristo. Kazi yake imepata umaarufu, pamoja na tuzo nne mfululizo za Dove Awards za mwanamuziki bora sana kwa wanawake, na kwa wimbo wake uliojulikana sana, "Held". Aliyezaliwa mjini Seattle,yeye sasa anaishi Nashville na mumewe, Bernie Herms. Alituzwa na Muungano wa Nyimbo za Kikristo tuzo ya Mwimbaji wa kike wa Mwaka katika miaka ya 2006, 2007, 2008 na 2009.

Natalie Grant

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Natalie Grant
Amezaliwa (1971-12-21)Desemba 21, 1971
Seattle, Washington
Aina ya muziki Nyimbo za kisasa za Kikristo
Kazi yake Mwanamuziki na Mtunzi wa Nyimbo
Ala Sauti
Miaka ya kazi 1999 hadi sasa
Studio Curb Records
Tovuti Tovuti Rasmi

Wasifu

hariri

Maisha ya awali

hariri

Natalie aliolewa na mzalishaji wa muziki Bernie Herms na alijifungua mapacha wasichana, Grace Ana na Isabella Noelle, tarehe 16 Februari 2007. Alikuwa msemaji na mtendaji kwenye ziara ya Revolve, mkutano kwa wasichana waliobaleghe ulioandaliwa na Wanawake wa Imani.

Albamu yake ya saba, Relentless, ilitolewa tarehe 12 Februari 2008. Vibao kadhaa kutoka albamu hii mpya viliimbwa katika ziara ya Revolve.

Alizuru hivi majuzi kwa ziara ya Speaking Louder Than Before akiwa pamoja na Bebo Norman na Jeremy Camp.

Diskografia

hariri

Albamu

hariri
  • Natalie Grant (1999)
  • Stronger (2001)
  • Deeper Life (2003)
  • Worship with Natalie Grant and Friends (2004)
  • Awaken (2005)
  • Believe (2005)
  • Relentless (2008)

Makala ya Waandishi

hariri

Tuzo za GMA Dove

hariri
  • 2006: Mwimbaji wa kike wa mwaka.
  • 2007: Mwimbaji wa kike wa mwaka.
  • 2008: Mwimbaji wa kike wa mwaka.
  • 2009: Mwimbaji wa kike wa mwaka.

Marejeo

hariri

1 ^ "GOSPEL MUSIC ASSOCIATION ANNOUNCES INITIAL HOSTS AND PERFORMERS FOR 41st ANNUAL DOVE AWARDS, TO BE HELD ON APRIL 21, 2010 AT NASHVILLE'S FAMED GRAND OLE OPRY® HOUSE". gospelmusic.org. 2009-12-23. http://www.gospelmusic.org/newsmedia/pressRoom_detail.aspx?iid=42151&tid=33 Ilihifadhiwa 25 Januari 2010 kwenye Wayback Machine..

2 ^ "Twins for Natalie". crossRhythms.co.uk. 2007-03-01. http://www.crossrhythms.co.uk/articles/news/Twins_For_Natalie/26341/p1/.

3 ^ "Shine FM::Matukio". 951shinefm.com. 2010-01-08. http://www.951shinefm.com/Dynamic/DynCon.aspx?cid=52&lpk=262 Ilihifadhiwa 7 Julai 2011 kwenye Wayback Machine..

Viungo vya nje

hariri