Nabii Nathani

(Elekezwa kutoka Nathani)

Nabii Nathani (kwa Kiebrania נתן הנביא) aliishi nchini Israeli kwenye mwaka 1000 hivi KK na habari zake zinasimuliwa katika Biblia, hasa 2Sam, 1Fal, 1Nya na 2Nya.

Nathan, kulia, na mfalme Daudi, walivyochorwa na Matthias Scheits.
Nathani akimlaumu Daudi.

Unabii wake

hariri

Kadiri ya Kitabu cha Pili cha Samueli, alikuwa nabii wa ikulu chini ya Mfalme Daudi.

Ndiye aliyemuarifu kwamba Mungu hataki amjengee hekalu la ajabu mjini Yerusalemu, halafu akamtabiria agano la pekee kati ya Mungu na yeye na uzao wake, likiendana na ahadi ya ajabu, yaani kwamba ufalme wake utadumu milele (2Sam 7).

Utabiri huo wa nabii Nathani ukaja kuongoza tumaini la Waisraeli hasa walipodhulumiwa, k.mf. zamani za Yesu chini ya ukoloni wa Kirumi, ambapo wote walimtazamia mwana wa Daudi mwenye kurudisha ufalme wa Israeli.

Ndiye pia aliyemlaumu kwa kuzini na Bethsheba, na kumuua mume wake, Uria Mhiti; halafu alimtabiria adhabu mbalimbali, hasa kwamba upanga hautaondoka nyumbani kwake (2Sam 11-12).

Kadiri ya vitabu vya Mambo ya Nyakati Nathani aliandika pia habari za utawala wa Daudi na wa mwanae mfalme Solomoni (1Nya 29:29 na 2Nya 9:29), na alishughulikia muziki wa hekaluni (2Nya 29:25).

Kadiri ya Kitabu cha Kwanza cha Wafalme (1:8-45) ndiye aliyemuarifu Daudi akiwa taabani kwamba mwanae mkubwa Adonia amejitangaza mfalme, akafaulu kumpatia nafasi hiyo mdogo wake Solomoni.

Nathani anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe 24 Oktoba au siku ya Jumapili ya Mababu Watakatifu, inayotangulia Noeli.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Nathani kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.