Nedokromili (Nedocromil), inayouzwa kwa jina la chapa Alocil miongoni mwa mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu mwasho unaotokana na mzio kwenye utando unaofunika sehemu nyeupe ya jicho.[1]

Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, macho kuwasha, na pua yenye kamasi linalotiririka.[1] Hakuna ushahidi wa madhara inapotumika katika ujauzito.[3] Ni kiimarishaji seli za kinga za familia ya tishu za uboho wa mfupa, ambayo hupunguza kuongezeka kwa histamini.[2]

Nedocromil iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1999.[1] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 230 kwa chupa ya mililita tano.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Nedocromil (EENT) Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "AHFS2021" defined multiple times with different content
  2. 2.0 2.1 "ALOCRIL (nedocromil sodium) solution/ drops". DailyMed. U.S. National Institutes of Health. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Mei 2014. Iliwekwa mnamo 17 Mei 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "PI2021" defined multiple times with different content
  3. "Nedocromil ophthalmic (Alocril) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Nedocromil Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)