Nefertiti

Malkia wa Misri na Mke Mkuu wa Kifalme (mke mkuu) wa Akhenaten, Farao wa Misri

Neferneferuaten Nefertiti (pia: Nofretete; mnamo 1370 KK   1330 KK) alikuwa malkia wa Misri ya Kale na mke mkuu wa Farao Akhenaten. Nefertiti na mumewe wanajulikana kwa mapinduzi ya kidini ambapo waliaanzisha ibada ya mmoja tu wakimwabudu Aten au Jua badala ya miungu mingi ya dini ya nchi. Wataalamu wengine wanaamini kwamba Nefertiti alitawala kama mfalme kwa muda mfupi baada ya kifo cha Akhenaten akitumia jina la Neferneferuaten na kabla ya utawala wa Tutankhamun. [1]

Sanamu mashuhuri ya Nefertiti - Nofretete
Sanamu ya Nefertiti akisimama iliyotengenezwa kwa mawe ya chokaa. Asili kutoka Amarna, sehemu ya mkusanyiko wa Misri wa Makumbusho ya Berlin .

Wakati wa uhai wa mumewe alitawala pamoja naye, hali ambayo haikuwa kawaida kwa wake wa mafarao.

Nefertiti amekuwa maarufu kutokana na sanamu ya kichwa chake kilichopo sasa katika makumbusho mpya ya Berlin, Ujerumani. Sanamu hiyo ni kati ya kazi za sanaa ya Kimisri zilizonakiliwa zaidi. Ilichongwa na mchongaji Thutmose ikapatikana katika karakana yake.

Marejeo hariri

  1. Van de Perre, Athena. 2014. "The Year 16 graffito of Akhenaten in Dayr Abū Ḥinnis: A contribution to the study of the later years of Nefertiti". Journal of Egyptian History 7:67-108.

Viungo vya nje hariri