New Times LA
New Times LA ni gazeti lakitambo lililokuwa likichapishwa kila wiki katika eneo la Los Angeles,California.Lilichapishwa na Shirika la New Times Media tangu mwaka wa 1996 hadi mwaka wa 2002. Mhariri mkuu wa muda wake wa kuchapishwa alikuwa Rick Barrs. Mwandishi Jill Stewart ndiye aliyekuwa anaandika makala ,yaliyoleta utata, ya kisiasa.
Katika mwaka wa 2002,New Times Media iliingia mkataba wa kutoshindana na shirika la Village Voice Media, shirika jingine cha uchapishaji magazeti ya kila wiki. Mkataba wao ulikuwa: kampuni hizo zingewacha kuchapisha magazeti ya New Times LA na Cleveland Free Times(gazeti la Village Voice Media) ili zisikuwe zikishindana katika mji wowote ule. Gazeti lililoshindana na New Times LA lilikuwa LA Weekly. New Times Media inaendelea kuchapisha majarida mengine mbalimbali kama Miami New Times,New Times Broward-Palm Beach na Phoenix New Times.
Mkataba huu ulifuatwa na upelelezi kutoka idara ya Haki ya Marekani. Uchunguzi ulisababisha malipo kutoka kampuni zote mbili,zikialazimishwa kuuza mali zao na magazeti yao ya kitambo kwa washindani wao.
Mali zao zilihusu vitu kama "samani ya ofisi, mifumo ya simu","haki zote za uchapishaji wa magazeti kwenye karatasi na pia ya kielektroniki", "leseni na vibali vya vituo vya usambazaji"na "orodha zote za wateja,mikataba,akaunti na rekodi za mikopo." [1]
Mali zote za New Times LA zilinunuliwa na kampuni ya Southland Publishing,Inc ambayo huchapisha magazeti kadhaa ya kila wiki ya mitaa. Kutoka kwa mali walizopata,Southland iliweza kuanzisha magazeti mawili: Los Angeles CityBeat na ValleyBeat. [2]
Angalia Pia
haririMarejeo
hariri- Howard Blume, The End of New Times, LA Weekly, Oktoba 4, 2002 Ilihifadhiwa 24 Agosti 2005 kwenye Wayback Machine.
- Savannah Blackwell, New Times Nailed: SF Weekly's Parent Company Charged with Violating Antitrust Law, San Francisco Bay Guardian, Januari 29, 2003 Archived 2014-01-11 at Archive.today
- [http://www.thenation.com/doc/20070716/wiener ^ End of an Era at the LA Weekly,[ Jon Wiener 27 Juni 2007, The Nation
- ^ Hold Separate Stipulation and Order : U.S. v. Village Voice Media, LLC and NT Media, LLC from US DOJ.
- ^ Southland Won't Compete Head-to-Head With LA Weekly from the Association of Alternative Newsweeklies's website, by John Ferri, 1 Julai 2003
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi ya New Times Media
- Tovuti rasmi ya Village Voice Media Ilihifadhiwa 23 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.