Ngai
Ngai ni jina analoitwa mungu katika kabila la Agikuyu nchini Kenya. Jina hili latumiwa pia kati ya Wamassai na Wakamba.
Kama ilivyo katika makabila mengineo ya Afrika Ngai hutolewa kafara, ni muumba, anauwezo dhidi ya viumbe na hata vitu visivyo kuwa na uhai na kadhalika. makazi yake kulingana na hadithi ya asili ya Agikuyu ni mlima Kenya (Kirinyaga). Kulingana na hadithi hii, Ngai alimuumba Gikuyu na mkewe Muumbi. Akawapa eneo la Muranga kama makazi yao. Akawabariki na mabinti tisa, kisha akaumba vijana tisa wa kiume iliwawaoe walipobaleghe. Kizazi baada ya kizazi jamii ya wakikuyu ilichipuka kutoka kwa nyumba hizi tisa. Majina ya Nyumba hizi hufanana na yale ya mabinti wa Gikuyu.
Marejeo
hariri- Leeming, David A. (2009). Creation Myths of the World (tol. la 2nd). ABC-CLIO. ISBN 978-1598841749.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help)
Viungo vya Nje
hariri- Ngai, The High God of the Kikuyu Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.