Nickson Akaba

bondia

Nickson Abaka ni bondia wa Kenya ambaye alifuzu kushiriki katika Olimpiki ya mwaka wa 2008 katika uzito wa "Welterweight" katika mchuano wa kufuzu wa Olimpiki wa Kiafrika wa 2 wa AIBA mwaka wa 2008.

Alimcharaza mpinzani wake Mehdi Kalsi katika nusu fainali ya kupambanua, lakini baadaye alibanduliwa nje na Mujandjae Kasuto katika fainali ambayo haikuwa na umaarufu na maana yoyote.

Hata hivyo, alikosa kushiriki katika Olimpiki kutokana na jeraha alilopata.

Marejeo hariri