Nicolaas Bloembergen
Nicolaas Bloembergen (amezaliwa 11 Machi 1920) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi. Mwaka wa 1958 alikata uraia wa Marekani. Hasa alichunguza mnururisho na usumaku wa kiini cha atomu. Mwaka wa 1981, pamoja na Arthur Schawlow na Kai Siegbahn alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nicolaas Bloembergen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |