Njuga
Njuga ni kifaa kama kengele ndogondogo zinazofungwa mguuni, mkononi au shingoni wakati watu wachezapo ngoma au mtoto aanzapo kutembea.
Ala hiyo ni bapa la chuma chepesi na lina umbo la duara na uwazi. Ndani huwekwa gololi ndogo ambayo inatoa mlio mkali inapotikiswa.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Njuga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |