Nothando Dube

Ufalme wa Swazi (1988–2019)

Nothando Dube (anajulikana kama Inkhosikati LaDube; 6 Februari 1988[1]– 8 Machi 2019) alikuwa mwanachama wa nyumba ya Dlamini kama Inkhosikati (Malkia mke) wa kumi na mbili na mke wa Mfalme Mswati III wa Eswatini.

Maisha Yake

hariri

Nothando Dube alikuwa Miss kijana wa Swaziland wa zamani.[2] Dube alisoma katika Shule ya Sekondari ya Mater Dorolosa.[3]Alikutana na Mswati III, mfalme wa Eswatini, mwaka 2004 katika sherehe ya kuzaliwa aliyoiandaa kwa ajili ya mmoja wa watoto wake. Aliamua kumuoa wakati wa ngoma ya manyasi aliyoshiriki pamoja na maelfu ya wanawake wengine wa Eswatini, iliyofanyika katika Kijiji cha Kifalme cha Ludzidzini.

Maisha kama mke

hariri

Mwaka 2005 aliolewa na Mswati III, akawa mke wake wa kumi na mbili, akiwa na umri wa miaka kumi na sita.[4] Alijifungua watoto watatu.[5][6] Mwaka 2010 alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Waziri wa Sheria Ndumiso Mamba, ambapo inasemekana aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani.[7][8][9] Aliwasilisha malalamiko ya unyanyasaji na mateso kutoka kwa walinzi wa mfalme.[10] Baada ya mwaka mmoja chini ya kifungo cha nyumbani, alifukuzwa kutoka katika familia ya kifalme na kupigwa marufuku kuwaona watoto wake.[11]

Alifariki mnamo tarehe 8 Machi 2019 katika hospitali nchini Afrika Kusini kutokana na saratani ya ngozi.[12][13] Kifo chake kilitangazwa rasmi na Gavana Lusendvo Fakudze kupitia Huduma ya Utangazaji na Habari ya Eswatini.[14] Alizikwa tarehe 11 Machi 2019.[15]

Marejeo

hariri
  1. Instagram
  2. Mebaley, Annie (28 Agosti 2014). "Who are the Queens of Swaziland?". ThisisAfrica. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-13. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "SWAZILAND". World of Royalty. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Mei 2018. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Eswatini mourns the death of King Mswati III's 12th wife". African Daily Voice. 9 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "King Mswati's 12th wife passes away". Mpumalanga News. 8 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "The King Of Swaziland and The Challenge of His Misbehaving Queens". Owlcation. 23 Mei 2018. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Minister caught red handed with King's wife". Nehanda Radio. 11 Agosti 2010. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Selander, Toby (7 Agosti 2011). "I am a prisoner, says Swaziland's Queen No 12". The Daily Telegraph. Telegraph Media Group. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Swaziland King's Wife Ladube (31) Dies, After Unhappy Life At Royal Palace". All Africa. 8 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Swazi queen flees to SA – report". Independent Online. Independent News & Media. 14 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Laing, Aislinn (20 Novemba 2011). "Twelfth wife of Swaziland kicked out of palace over 'affair' with justice minister". The Daily Telegraph. Telegraph Media Group. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "King Mswati's twelfth wife dies". The Citizen. 8 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. Samanga, Rufaro (8 Machi 2019). "The Twelfth Wife of King Mswati III of eSwatini has Died". Okay Africa. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "King Mswati's 12th wife has died". SABC News. South African Broadcasting Corporation. 8 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. Shange, Sibusiso (8 Machi 2019). "INKHOSIKATI LADUBE PASSES ON". Times of Swaziland. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-11. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)