Nusinerseni
Nusinerseni (Nusinersen), inayouzwa kwa jina la chapa Spinraza, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa seli za neva kwenye uti wa mgongo zinazodhibiti mwendo wa misuli (spinal muscular atrophy).[1] Dawa hii inaboresha kazi ya uwezo wa mfumo wa neva kudhibiti na kuratibu harakati za hiari na zisizo za hiari za misuli ya mwili.[1] Inatolewa kwa njia ya sindano kwenye mfereji wa uti wa mgongo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maambukizi ya njia za kupumua, kuvimbiwa choo na maambukizi ya sikio.[1] Madhara yake mengine ni pamoja na kupungua kwa pletleti za damu, kutokwa na damu na matatizo ya figo.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Ni asidi ya nyuklia ya aina ya antisense oligonucleotide ambayo huongeza kazi ya jeni inayotengeneza protini ambayo ni muhimu kwa maisha na utendakazi wa niuroni za mwendo (motor neuron), ambazo ni seli za neva zinazohusika na harakati za misuli.[2]
Nusinerseni iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2016 na Ulaya mwaka wa 2017.[1][3] Nchini Uingereza, inagharimu takriban £75,000 kwa dozi kufikia mwaka wa 2021.[2] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu takriban dola 133,000 za Kimarekani.[4]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Nusinersen Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1170. ISBN 978-0857114105.
- ↑ "Spinraza". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Spinraza Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nusinerseni kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |