Nyanda za chini za Turan

Nyanda za chini za Turan (kwa Kiingereza: Turan Depression, Turanian Basin) ni eneo tambarare la km² milioni 1.9 lililopo duni kuliko mazingira yake katika Asia ya Kati. Linaenea katika Turkmenistan kupitia Uzbekistan hadi Kazakhstan, tariban baina ya Bahari ya Kaspi na Ziwa Aral. Asilimia 80 ni jangwa la mchanga au la chumvi.

Ramani ya bahari ya Kaspi na Ziwa Aral, kivuli cha manjano kinaonyesha beseni la Kaspi.

Mvua ni haba na uoto ni mimea midogo, nyasi na vichaka vidogo vinavyofaa kama lishe ya kondoo na ngamia lakini penye oasisi watu wamekuwa wakilima pia tangu kale.[1].

Kwa wastani, eneo hilo hupata chini ya mm 381 za mvua kwa mwaka. Jangwa la Kara Kum linapatikana kusini mwa Nyanda za chini za Turan.

Miji mitatu mikubwa zaidi ni: Daşoguz huko Turkmenistan, Nukus katika Uzbekistan, na Urganch, pia katika Uzbekistan.

Sehemu za chini zaidi ziko Turkmenistan zikiwa mita 81 chini ya usawa wa bahari .

Mito ya Amu Darya na Syr Darya hutiririsha maji kutoka milima ya Pamir na Tien Shan hadi Ziwa Aral kuvukia majangwa haya.

Kimataifa eneo lina umuhimu wa kiuchumi kutokana na akiba za gesi asilia na mafuta ya petroli katika mazingira ya Bahari Kaspi[2].

Marejeo hariri

  1. Ecological research and monitoring of the Aral Sea Deltas: a basis for restoration, uk. vi
  2. Oil-Gas Prospects of the North Turan Zone of Downwarps, tovuti ya Petroleum Geology: A Digest of Russian Literature, ilitazamiwa Novemba 2019
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za chini za Turan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

41°50′00″N 59°58′00″E / 41.8333°N 59.9667°E / 41.8333; 59.9667